Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2013

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Hadi majira haya ya  saa 1.45 leo asubuhi,  Uhuru ambaye ni mgombea wa TNA alikuwa amepata kura 2,355,726 wakati Raila ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 1,576,765.
 Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) inataraji kutoa matokea rasmi ya Urais kesho Ijumaa.
Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.
Wagombea wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed Dida na  Paul Muite.

BOFYA MATOKEO KENYA  KUONA MATOKEO HAYO LIVE 
Posted by MROKI On Thursday, March 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo