Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2013

 Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake

**********
 Magari yalifukiwa na kuharibika vibaya
 Vijana walikuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo nao walijeruhiwa vibaya
Zege kama hili kwa mikono tu bila vifaa vyauhakika ni ngumu kulitoa.
TAARIFA YA UHAKIKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 16 LILIPO JIRANI NA MSIKITI WA SHIA ULIOPITA KATIKA MTAA WA IDRA GHAND,KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM,LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA 

INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.

MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI. AIDHA UHABA WA VIFAA VYA UOKOAJI UNAWEZA KUCHELEWESHA ZOEZI HILO LA UOKOAJI. MINONGONI MWA VIFAA VINAVYOHITAJIKA HAPO NI PAMOJA NA MASHINE ZA KUPASULIA ZEGE, SCAVETA KWAAJILI YA UFUKUAJI.
 CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.

PICHA NA VIDEO ZA TULIO HILO LA KUSIKITISHA ZITAWAJIA PUNDE TU,HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO. SOURCE: MICHUZI MEDIA
Posted by MROKI On Friday, March 29, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo