Kiongozi
mkuu maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi
mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya
Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa
jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya
Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.
Akitangaza
zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa
polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo
tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano
hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa
waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo.
Mshindi
wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi set
moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata
pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet)
15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata pesa taslimu shilingi
laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,Aidha
zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo kila
mmoja atapata pesa taslimu shilingi laki moja, vocha za kufanya
manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1.Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.
Mashindano
ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha
Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home
Shopping Center pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,
ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za
usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la
kuendelea kudhibiti ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi
jamii.
Mashindano
haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya
Polisi Oysterbey kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga
Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye
kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm. SOURCE: JIACHIE BLOG.
0 comments:
Post a Comment