"MIKOA ya Mbeya na Dodoma imechomoza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka 2013", Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kuongezwa
kwa mikoa hiyo kunaifanya idadi ya mikoa ambayo tamasha hilo
litafanyika kwa mwaka huu kufikia mitano.
Msama
alisema baada ya Tamasha la Pasaka kufanyika Dar es Salaam Machi 31,
siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, kisha Aprili 2 ni
Uwanja wa Samora Irringa. “Aprili 6 itakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma na
siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Hiyo ni mikoa
ambayo mashabiki wameipigia kura kwa kiasi kikubwa tamasha lifanyike
maeneo hayo.
“Tunaamini
mashabiki wetu watapata fursa nzuri ya kufurahia tamasha hilo, ambalo
mwaka huu tumepanga mikoa saba tutumbuize, lakini bado tunaangalia mikoa
mingine miwili,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza kuwa
kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wachague
tamasha hilo lifanyike wapi mwaka huu na kuwa mikoa hiyo ndiyo
iliyopendekezwa zaidi.
Wakati
huohuo, Msama alisema baadhi ya wasanii tayari ameanza kumalizana nao
kwa ajili ya tamasha hilo na kuwa wakati wowote kuanzia leo wataanza
kutangazwa rasmi.
0 comments:
Post a Comment