Mahmoud Ahmad,Arusha
TANZANIA imepata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii vya Mlima
Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti ambayo ndio
iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi nyingine yeyote.
Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa rais
wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa nchini Marekani
mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kutokana na Tanzania kuwa na
vivutio vya kipekee ndio sababu iliyopelekea kupata ushindi huo.
Akielezea
hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee
iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama
wanaohama kwa msimu.
Naye
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo
alisema kuwa nchi za Afrika zinavivutio vingi vya utalii na fursa kubwa
ya kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema anaamini kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivuti vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.
“Afrika ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Alisema kwa Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika ambazo
ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa
ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
Pinda.
Alisema
kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio
vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dk, Alan Kijazi alisema mlima
Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya
kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Akizungumzia
kuhusiana alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama
wa kila aina kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe
na Mamba.
Mbali
na Tanzania Dk.Imler alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni
Red sea Reefs, Okavango Inland delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara
Desert na River Nile.
Aidha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ushindi huo ni
historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
0 comments:
Post a Comment