Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2013



Hatimaye Ndugu Jamaa na Marafiki waishio Jijini Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wenzake na Marehemu Grace Mathew Chao leo wametoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Mpendwa wao Grace katika zoezi lililofanyika Katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam ambako mauti yalimkuta Februari 17, 2013. Grace Chao alizaliwa Desemba 13, 1985.

Mwili wa Grace ulisafirishwa kuelekea Mazimbu Mkoani Morogoro ili kuwapa fursa wana jamii ya Mazimbu na Mzumbe ambako marehemu alizaliwa na kuishi zoezi ambalo litafanyika kesho Jumatano kabla ya Msafara kuelekea Marangu kwa mazishi. Ungana na Father Kidevu Blog katika tukio hilo.
 Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kazi na masomo walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.
 Mama wa Marehemu Grace (kushoto) akiwa na mwana familia mwingine wakati wa zoezi hilo leo.


Ilikuwa ni majonzi sana katika tukio hili, kwa Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.

 Wafanyakazi wa CRDB Bank waliita kutoa heshima kwa Mwili wa Mfanyakazi mwenzao.
 Vijana wa Mzumbe Wengi sana walijitokeza kumuaga Grace katika safari yake hiyo ya Mwisho.
Marafiki na vijana wa Mzumbe wakimfariji kaka wa Marehemu Edwin Ndesamburo Chao (kulia) kufuatia msiba wa dada yake.
Posted by MROKI On Tuesday, February 19, 2013 6 comments

6 comments:

  1. Still unbelievable!
    Rest in peace my friend Grace.

    Asante Mroki kwa kutupa habari tulio mbali. Nawashukuru pia wanamzumbe wanaotuwakilisha huko.

    Tuko pamoja.
    Irene Katalyeba.

    ReplyDelete
  2. Mungu ailaze roho yake mahali pema amina

    ReplyDelete
  3. Rest in Peace Grace

    ReplyDelete
  4. rest in peace Grace

    ReplyDelete
  5. Mungu ni mwema kwa kila jambo. poleni sana wanafamilia wote.R.I.P Grace

    ReplyDelete
  6. Mm nimesoma mzumbe ila huyu dada simkumbuki ila nawaona tuliosoma nao alisoma mwaka gani naona bado mdogo she wa so young to die na ndio alianza kuchuma alichopanda mama mzazi lazma amelia sana nguvu kazi za taifa zina zidi kupotea may her soul rip.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo