Na Mwandishi wa EANA
Arusha, 5 Februari,2013 (EANA) Afisa Mkuu
Mwandamizi wa Msuala ya Anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
Ladislaus Matindi amesema mchakato wa usafiri huria wa anga katika kanda ya ya
EAC unaendelea vizuri na kwamba jumuiya inatarajiwa kuuchambua mswada husika
mwishoni mwa Mei, mwaka huu.
‘’Kutokana na maendeleo yaliyopo, inatarajiwa
kwamba operesheni ya kuleta tija na kuongeza fmasafa na uwezo litatuongoza
katika hatua ya juu ya utoaji huduma katika soko ya anga katika kanda na pia
kupunguza nauli na gharama za kusafirisha mizigo,’’ alithibitisha Matindi.
Mapema mwaka 2006, Mkutano wa 11 wa Baraza la
Mawaziri la EAC lilifanya mabadiliko makubaliano yaliyopo ya Usafiri wa Anga
(BASAs) baina ya nchi kuhusu kuondoa vikwazo vya uwezeshwaji na masafa , kuwa
ni hatua za awali kabisa katika utekelezaji wa mpango huo.
Matindi aliendelea kusema kuwa eneo
la kuanzia kwa EAC katika juhudi zake za kuanzisha usafiri huria katika soko la
anga ni uamuzi wa baraza la mawaziri kuhusiana na utekelezaji wa azimio la
Yamoussoukro la Oktoba 7, 1988 juu ya kufanya usafiri wa anga katika soko la
Afrika kuwa huria, jambo ambalo halijatekelezwa.
Afisa huyo wa EAC alirudia kwamba kwa kuzingatia
utekelezaji wa azimio hilo katika kanda ya EAC na matumizi ya makubalino ya
Soko la Pamoja, nchi wananchama wa EAC zitaweza kuiondoa zenyewe vikwazo dhidi
ya maendeleo ya sekta ya anga vinavyohusiana na uwezo, masafa,uhujumu na
uchaguzi wa makampuni ya ndege.
Alisema changamoto ambayo ya wazi kabisa ni ya
uhakika kuwepo kwa biashara ya ushindani uliosawa kati ya kampuni ndogo za
usafiri wa anga na makubwa .
0 comments:
Post a Comment