Rais
Jakaya Kikwete leo amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi wilayani Uvinza
mkoani Kigoma.
Rais
Kikwete alitembelea daraja hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na
daraja hilo na kuwataka walitumie vyemka katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni
pamoja na kutumia ardhi yao kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.
Kikwete
amewaambia wakazi hao kuwa wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama
wawekezaji na kununua maelfu ya hekta za ardhi yao.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia daraja jipya lililojengwa katika Mto Malagarasi.
Rais Kikwete na Msafara wake wakiimbiwa nyimbo za pongezi na kundi la ngoma Malagarasi.
Uhondo wa Ngoma ni kuingia kucheza...Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akicheza ngoma ya akina mama wa Malagarasi Uvinza.
Rais Kikwete na Mkewe wakipiga picha ya kumbukumbu
Ukaguzi ukiendelea
Rais Kikwete akisifu ubora wa ujenzi wa daraja hilo.
Rais Kikwete na Mkewe walipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Malagarasi na kuwaasa juu ya kuilinda ardhi yao na kulitumia vyema daraja hilo.
Rais wakati akitoka Malagarasi alikutana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano Uvinza Kibaoni na kusalimiana nao.
Wakazi wa Simbo nao walipata fursa ya kuzungumz na Rais Kikwete.
Wananchi wa Kazuramimba nao walisalimiwa na Rais Kikwete na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Fares Jairos alisema kero zao na Rais kuahidi kuzitatua kubwa ikiwa ni Ujenzi wa Zahanati.
Wakazi wa Uvinza nao walimsimamisha Rais Kikwete na kuzungumza nao. Kilio kikubwa walicho kishikia bango ni Mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Chumvi Uvinza na Umeme.
0 comments:
Post a Comment