Waandaaji
wa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba
mbio za mwaka huu zitafanyika katika njia zile zile zilizotumika mwaka
jana. Mbio hizo limepangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu mjini Moshi.
John
Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, ambao ni waandaaji wa
tukio hilo alisema katika taarifa jana kwamba njia zitakazotumika kwa
ajili ya Kilimanjaro Marathon2013 ni kuanzia Uwanja wa chuo cha Ushirika
(MUCCoBS) kuelekea katikati ya mji, na kisha kufuata barabara kuu ya
kwenda Dar es Salaam kwa takriban kilomita 8 hadi 9, baadaye watageuka
na kurudi Moshi mjini kupitia katikati ya mji, na badaaye watapandisha
mwinuko kidogo kuelekea Mweka, “wanariadha watafurahia zaidi sehemu hii
kwasababu ina mandhari ya kuvutia na kutakuwa na washangiliaji wengi
kando ya barabara”.
Addison
anasema, “sehemu ya kupandisha kuelekea Mweka inahitaji kupanda kwa
taratibu lakini kwa sababu Mlima Kilimanjaro ni kivutio na uwepo wa
wananchi wanaoshangilia muda unaenda haraka na kuwasaidia wakimbiaji
kumaliza mapema”.
Alisema
kuwa kituo cha cha Mweka ambapo ndipo wanaridha waatakapogeukia ili
kurudi uwanja wa Ushirika inakuwa ni takribani kilometa 32 tangu kuanza
mbio ndefu ya kilomita 42. Baada ya hapo kipande kilichobaki inakuwa ni
mteremko kuelekea uwanjani mwisho wa mbio na njia nzima ni mteremko tu.
Aliongeza
kuwa kwa wale watakaoshiriki nusu Marathon, mbio zitaanzia uwanja wa
MUCCoBS ambapo pako tambarare na baadae watapandisha kwenye mwinuko
kidogo kuelekea Mweka kama ilivyo zile mbio ndefu kabla ya kurudi umbali
wa takriban km 10, kuelekea tena uwanjani.
Kutakuwa na
meza za maji kama ilivyo kawaida na magari maalum ya kunyunyizia maji
mithili ya mvua kando ya barabara huduma ambazo zimeandaliwa maalum
kuwafanya wanariadha waendelee kuwa na nguvu wakati wote wa mbio hizo.
Kuhusu
burudani, Addison alisema kuwa hali ya uwanjani itakua ya kusisimua
kutokana na burudani kali kutoka bendi za muziki wa nyumbani
zitakazokuwepo, chakula cha kutosha, nyama choma na vinywaji na bila
kusahau mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run ambazo pia
zinatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake.
“Ili
kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara zitakuwa
zimefungwa, asubuhi siku ya mbio, lakini kutakuwepo na njia mbadala
kuzunguka mji kwa ajili ya wakazi wa Moshi. Wakazi wa Moshi ambao
wanatarajia kukimbia pamoja na wakimbiaji wengine watakaofika Moshi
mapema wanaweza kuanza mazoezi katika njia hizo hili kupata uzoefu wa
njia na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mbio.”
Mbio hizo
zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro
PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na Vodacom
Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement,
CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New
Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Idadi ya Watu (UNFPA).
0 comments:
Post a Comment