Kwa nusu
karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari za uhakika kwa
lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya Mashariki mwa
Afrika na eneo la Maziwa Makuu. Tarehe 22 Februari, saa 9.oo mchana katika
jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea maadhimisho haya kwa hafla
maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwa- leta pamoja wachambuzi
wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya “ Maarifa na Mwamko kupitia
Vyombo vya Habari“.
Hotuba
maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea
Schmidt.
“Idadi
kubwa ya wasikilizaji wetu wanaishi hapa Tanzania, kwa hivyo lilikuwa chaguo la
uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea Schmidt. “Kwa miaka 50
iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari zenye uwiano na taarifa za
uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki habari na uchambuzi wa kina juu ya
masuala yenye uzito mkubwa.“
Uchambuzi
utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada wa Shirika la
Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na utafanywa kwa lugha ya
Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza majadiliano hayo akiwa na wataalamu
wa vyombo vya habari wanaoheshi- mika nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew
Mwambene (Mkurugenzi
wa Idara
ya Habari, Maelezo), Mohamed Abdulrahman (DW), Jenerali Ulimwengu (Mwandishi wa
habari), Valerie Msoka (Mkurugenzi wa TAMWA) na Maggid Mjengwa (Mtaalamu wa
mitandao ya kijamii).
Wahudhuriaji
watakuwa pia na fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na waandishi wa DW
kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Tanzania, ambao wanahudhuria hafla hiyo katika jengo la Makumbusho ya Taifa.
Katika
kufanya taarifa ziwe na maana
Idhaa ya
Kiswahili ya DW hutangaza mara tatu kwa siku kwa ajili ya maeneo ya Afrika ya
Mashariki na Maziwa Makuu. Ikishirikiana na redio washirika zinazotangaza kwa
masafa ya FM kwenye eneo hilo, DW inaweza kuwapa wasikilizaji habari zenye
uwiano juu ya kile kinachoendelea ulimwenguni kwa ujumla na hasa yale
yanayoendelea barani Afrika. Ili kupata mtazamo huu wa kimataifa, timu ya
waandishi wa habari kutoka mataifa matano ya Kiafrika inafanya kazi na mtandao
wa wawakilishi wetu walioko kote Afrika Mashariki na Kati.
Idhaa ya
Kiswahili ni moja ya idhaa mashuhuri sana za DW. DW ina kipindi cha kuelimisha
kilichoshinda tuzo kadhaa cha “Noa Bongo! Jenga Maisha Yako!“ na makala za aina
mbalimbali zinazogusa masuala ya afya, haki za binaadamu, mazingira, wanawake
na maendeleo, vijana na mitindo ya maisha na utamaduni.
0 comments:
Post a Comment