Na Ben
Komba, FK BLOG Pwani
CHAMA
kinachofanya utafiti juu ya watu wasiosikia nchini, (TADERE) kimefanya warsha
maalum kwa wazazi na walimu wenye watoto walemavu na maofisa watendaji wa
vijiji katika kuboresha mazingira ya kijamii kwa watu wasiosikia ambao wamekuwa
wakipitwa na mambo mbalimbali kutokana na hali yao.
Mkurugenzi
wa TADERE, Nidrosy Mlawa amesema watu wenye matatizo ya kusikia wamekuwa
wakiachwa nyuma katika masuala mbalimbali kutokana na ukosefu wa wakalimani wa
kutosha kuwatafsiria matamko mbalimbali yanayotolewa na serikali na kusababisha
ushiriki wao kuwa mdogo kama katika mchakato wa katiba mpya unaooendelea.
Mlawa
amebainisha jamii lazima ikumbuke kuwa walemavu wa kusikia nao wana wajibu wa
kupata huduma za kiroho na hivyo ameshauri wakati sasa umefika kwa madhehebu ya
dini mbalimbali kuweka mazingira ambayo yatamuwezesha mtu asiyesikia kupata
huduma hiyo ya kiroho.
Naye
kamishna mstaafu wa ustawi wa jamii Tanzania, Nnyapule Madai ambaye alikuwa
mwezeshaji katika warsha hiyo amewaambia washiriki kuwa kipindi cha azimio la
Arusha suala la kushughulika na walemavu lilikuwa ni la serikali, na
liliwazungumzia kama ni kundi ambalo linahitaji kulelewa sawa na watoto na
wazee na wengine wote ambao maumbile yao yanawafanya washindwe kufanya shughuli
za uzalishaji mali.
Madai
amefafanua kwa sasa Tanzania ina walemavu takriban milioni 4 ikiwazingatia
sensa ya mwaka 2012, lakini changamoto kubw wanazokabiliana nazo ni Walimu
wengi kutokuwa na utaalamu wa kugundua watoto wenye matatizo ya kusikia na
baadhi ya vyuo vya ufundi kukosa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu wa
aina yoyote ile.
Madai
ameongeza kuywa kukosekana kwa nyenzo za kujimudu kwa watu wenye ulemavu kama
Vikuza sauti kwa watu wasiosikia, fimbo nyeupe kwa walemavu wa kuona, na mafuta
ya kujipaka, miwani na kofia kwa ajili ya watu wenye walemavu wa ngozi na viti
vya magurudumu kwa walemavu wa viungo, Aidha amezitaka taasisi ambazo zinatoa
misaada kuhakikisha zinatoa vifaa vyenye ubora unaotakiwa badala ya kuwapatia
vifaa ambavyo vingi havidumu hata miezi mitatu vinaharibika hasa upande viti
vya magurudumu.
0 comments:
Post a Comment