Wajumbe wa sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana leo
wameanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma kwa njia ya reli ya Kati.
Wajumbe hao wanne, Kinana, Katibu wa Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa Organization, Dk. Mohamed Seif Khatib, Katibu wa
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro wameanza safari hiyo
mchana wa saa 8:30 ikiwa ni moja ya Harakati za kuiunga mkono serikali kufufua
usafiri huo muhimu kwa watu wa Kanda ya Magharibu kwa Mikoa ya Shinyanga,
Tabora na Kigoma.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda treni
hiyo, Kinana alisema ufufuaji wa reli ya Kati ni moja ya Ilani za Chama cha
Mapinduzi katika utekelezaji wa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Pia
wamelipongeza Shirika la Reli nchini kwa ufanisi wa haraka kwa kufufua reli
hiyo.
Nape akiagana na wana CCM mkoa wa Dar es Salaam
Abiria wakiwa katiaka Behjewa la 3rd Class
Katibu Mkuu wa CCM alipokuwa akielekea kuapanda Treni
Wana CCM Dar es Salaam walipoisindikiza Secretarieti
Katibu Mkuu wa CCM akisoma kitabu ndani ya treni wakati wa safari
Nape akiwa chumbani kwakwe
Dk. Khatibu akizungumza na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Madabida
0 comments:
Post a Comment