Meneja
Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo
wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu
ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni
ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel
Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG, Prosper
Vedasto.
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya
shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya
wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
Hayo
yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo
katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media
group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic
FM.
Rugambo
alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao
wegi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia
katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba
15678 na kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku
ya Valentine.
“Hii ni
promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari,
lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile
vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa
taifa,” alisema Rugambo.
Alisema
kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata
nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs
milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000
na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa
mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao
kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha
ya kila siku.
Alisema
kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza
kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema
kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha
zaoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment