Mbunge wa Jiji la Arusha Godbless Lema amelipongeza jeshi la
polisi mkoani hapa kwa kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu wakati wa kipindi
cha sikukuu za mwisho wa mwaka na kulitaka jeshi hilo kutoa ushirikiano kwa
wananchi sanjari na kuacha kazi za siasa na badala yake kazi ya siasa kuziachia
CCM na Chadema.
Lema aliyasema hayo wakati alipofika kwenye ofisi yake kwa
mara ya kwanza tangu mahakama kuu ilipotengua matokeo ya ubunge wake hadi
mahakama ya rufaa ilipomrudishia ubunge huo mwisho mwaka jana.
Alisema kuwa kazi za siasa wanatakiwa kuachiwa wanasiasa na
jeshi la polisi kusimamia uvunjifu wa amani na kuwa maandamano ni haki ya
kikatiba wao kuwazuia watakuwa hawatendi haki na huko ni kuwanyima walio wengi
kupaaza sauti zao dhidi ya ukandamizaji.
Mh. Lema alisema kuwa kila mtanzania anahaki ya msingi katika
kudai haki ila wao kwa sasa hawataandamana hadi pale watakapoona kuna uvunjaji
wa haki za wananchi ndipo nguvu ya umma itakapotumika na kuwasihi polisi kutoa
ushirikiano kwa wakazi wa jiji hilo na vyama vyote vya siasa.
Aidha mh,Lema alisema kuwa viongozi wa serekali wanatakiwa
kuacha kuwaburuza wananchi wa kipato cha chini wanaojishulisha na biashara za
umachinga na badala yake kuwatengea maeneo ya kufanyia shughuli zao za
kujipatia riziki za watoto wao kwa kuwaonyesha mahala pa kwenda badala ya
kutumia mgambo kuwapiga mama zao.
Alisema kuwa atakaa na viongozi kujadili njia sahihi za
kutatua kero hiyo ili kusitokee manung’uniko kutoka kwa wananchi hasa wasio
kuwa nacho pia alisema kuwa kabla hajafika kwenye ofisi hiyo alipata taarifa
kuwa kwenye ofisi hiyo kumewekwa madawa ya kulevya ili waweze kumkamata nayo
atakapofika kwenye ofisi hiyo.
0 comments:
Post a Comment