Msafara wa
Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, ukiongozwa na Katibu Mkuu,
Abdulrahaman Kinana kuelekea Mkoani
Kigoma katika maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi umefika
salama Mkoani Tabora usiku huu na kupata
Mapokezi makubwa kutoka kwa wana CCM mkoani hapo.
Msafara
huo ulio na Wajumbe hao wane wa Sekretarieti ya CCM, na wanahabari pamoja na
maofisa kadhaa wa Chama hicho ulizna safgari yake jijini Dar es Salaam Januari
25, 2013 majira ya saa 8:30 jioni na kusafiri usiku mzima njiani hadi kufika
Mjini Tabora majira ya saa moja na nusu 1:30 Usiku.
Mapema
mchana msafara huo ulipata mapokezi makubwa katika Stewsheni ya Saranda ambapo
viongozi hao baada ya kuhutubia wana CCM walijichanganya na abiria wengine
kupata chakula cha mchana.
Kinana
aliwaambia wenyeji ambao walikuwa wam,eandaa chakula kwaajili yao kuwa watakula
kinachouzwa na wakazi wa hapo kuchangia kipato chao kama wasafiri wengine.
Hakuna kujivunga hapa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai akimpokea Katibu Mkuu wa CCM.
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiteremka katika treni.
Katibu Mkuu wa CCM akiongozana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai ambaye ni Mwenyekiti (wapili kulia) na Naibu Katibu Mstaafu, John Chiligati.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa Skafu na Chipkizi wa CCM Saranda,
Derick Chongole mara baada ya kuwasili eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment