Nafasi Ya Matangazo

December 11, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa kata ya Mao waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara akiwa ziarani Mkoani Rukwa kuhamasisha kilimo na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwepo chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto walio chini ya miaka mitano, elimu, utawala bora na kampeni ya ondoa nyasi weka bati ijulikanayo kama "Onyaru" Ondoa nyasi Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kata ya Legezamwendo Wilayani Kalambo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli mbalimbali za maendeleo. Katika kata zote 13 alizotembelea wananachi walijitokeza kwa wingi ambapo pia walipewa fursa ya kuuliza maswali na kuwasilisha kero zao. Maswali na kero zao zilipatiwa ufumbuzi na nyingine kupewa muda kushughulikiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Mshani kwenye ziara yake ya kuhamasisha kilimo na shughuli mbalimbali za kimaendeleo Mkoani humo. Wananchi wengine walilazimika kupanda juu ya miti ili kuweza kupata ujumbe vizuri.

Ziara hii ya Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa ilienda sambamba na zoezi la chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto waliochini ya miaka mitano. Pichani ni Dkt. Edina Yesaya ambaye ni kaimu mganga mkuu wa Halamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga akitoa chanjo kwa mmoja ya watoto waliofika kupata chanjo hiyo. Watoto zaidi ya 2000 wamepata chanjo hiyo katika kata na vijiji 13 msafara huo ulipopita.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akisisitizia jambo kwa wananchi wa kata ya Kilembe. Aliwataka wananchi kwa kushirikiana na uongozi wa kata na watendaji kushirikiana kuhakikisha miundombinu katika shule ya Msingi Kilembe inaboreshwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akimkaribisha kwa shangwe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ili aweze kuzungumza na wananchi wa Kata ya Legezamwendo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Muimbaji wa kikundi cha kwaya cha Last kutoka Kata ya Legezamwendo akiimba kwa staili ya aina yake huku akisalimiana na viongozi waliokuwepo meza kuu. 
Mambo yalikuwa hivi katika makao makuu ya Wilaya mpya ya kalambo. Wananchi walifurika kwa wingi. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwata viongozi na wananchi wa Wilaya hii mpya kuzingatia kujenga mji wao kwa kuzingatia mipango miji iliyo bora pamoja na kusisitizia suala la usafi ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Moshi Chang'a ameteua siku ya jumamosi ya kila wiki kuwa siku ya usafi kwa Mji mzima wa Matai ambao ndio makao makuu ya Wilaya ya Kambo.

 Wananchi walipewa fursa ya kuuliza maswali na kutoa kero zao.

Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bwana Ngindo akifurahia jambo na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Frank Mateni na Afisa Kilimo kwenye dawati la uwekezaji Bwana Misasi Marco kwenye ziara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na madereva wa bodaboda katika Mji mdogo wa Laela katika ziara yake Mkoani Rukwa ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli nyingine mbalimbali za kimaendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akigawa "Reflectors" kwa madereva wa bodaboda katika Mji mdogo wa Laela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo anafanya ziara katika Mkoa huu kuhamasisha kilimo bora katika msimu huu wa kilimo pamoja na shughuli nyingine za kimaendeleo. Mkuu huyo wa Mkoa aliwaasa vijana hao kujenga umoja wenye nguvu kwani utawasaidia pia kupata mikopo mbalimbali. Aliugiza uongozi wa halmashauri kuwapimia viwanja madereva hao ambao wapo 22 viwanja ambavyo watavilipia wao wenyewe. 
Zaidi ya asilimia 70% ya wakulima Mkoani Rukwa hutumia jembe la kukokotwa na wanyama katika shughuli zao za kilimo. Mkulima katika kijiji cha Matanga akiandaa shamba lake kwa ajili ya kupanda mazao katika msimu huu mpya wa kilimo cha mvua wa mwaka 2012.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akiwaimbisha wananchi wa Kata ya Kilembe Wilayani Kalambo ikiwa ni kuwaweka sawa kwa ajili ya kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyepo kwenye ziara ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli pamoja na miradi mbalimbali ya maenedeleo.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview blog)
Posted by MROKI On Tuesday, December 11, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo