Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter
Muhongo (wa kwanza kushoto), na Naibu wake Mhe. Stephen Masele wakishiriki
katika mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika hivi
karibuni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini, Mhe. Stephen Masele akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka
wa wachimbaji wadogo wa madini nchini, uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
Uongozi wa mpito kitaifa wa Chama cha Wachimbaji Wadogo
wa Madini mara baada ya kuchaguliwa na
mkutano wao mkuu wa mwaka uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini,
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto), na Naibu wake Mhe. Stephen
Masele wakishiriki katika mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini
uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini,
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) katika picha ya pamoja na makamishna
wasaidizi wa madini kutoka kanda mbalimbali, mara baada ya kufunga mkutano mkuu
wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
*********
Wizara ya Nishati na Madini
imetenga jumla ya shilingi bilioni 8.9 kwa dhamira ya kuwainua wachimbaji
wadogo wa madini nchini ili kukuza kipato chao na hivyo kuboresha maisha yao.
Aidha, jitihada za kuwainua
wachimbaji wadogo zinalenga pia kuinua pato la taifa kutokana na kuongezeka
kiwango cha kodi na tozo mbalimbali zinazopaswa kulipwa na wachimbaji hao kwa
serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wajumbe
waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini nchini,
uliofanyika mjini Dodoma tarehe sita na saba mwezi huu.
“Tunayo dhamira ya dhati
kuwasaidia ili maisha yenu yaboreke na pia ili kukuza pato la taifa hili”,
alisisitiza Waziri Muhongo na kuongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) ndilo limepewa jukumu la kusimamia mipango ya uendelezaji wachimbaji
wadogo kwa kushirikiana na taasisi nyingine mbalimbali zinazohusika na sekta ya
madini.
Hata hivyo Profesa Muhongo
amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini kuhakikisha wanasajili biashara
zao, kuanisha mapato yao, pamoja na kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazowahusu
ili taifa liweze kunufaika na rasilimali hiyo ya madini.
Alisisitiza kuwa wachimbaji watakaofuata
vigezo hivyo ndiyo tu watakaopata misaada ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo na
mikopo kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo.
Kwa upande wao, wajumbe
waliohudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambao ni viongozi na wawakilishi wa
vyama vya wachimbaji madini kutoka mikoa yote nchini, waliahidi kuyafanyia kazi
maagizo hayo ya Waziri kwa manufaa yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment