TUSKER ya Kenya, jana iliwaacha mashabiki wa Yanga vichwa chini
baada ya ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Wanajangwa hao katika mchezo wa
kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Yanga iliwajaribu wachezaji
wake kadhaa iliyowasajili kipindi cha dirisha dogo, huku pia wachezaji
chipukizi wakipewa nafasi kwa mara ya kwanza.
Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alisema pamoja na
kipigo hicho, amefurahishwa na kiwango walichoonyesha wachezaji wake
kwenye mchezo huo.
“Matokeo siyo mazuri, lakini nimeridhika na
kiwango walichoonyesha wachezaji wangu [Kabange Twite] amecheza vizuri
ingawa ni mechi yake ya kwanza,” alisema kocha huyo.
Iliwachukua Tusker dakika tano kulitia hekaheka
lango la Yanga, na wangeweza kuwa mbele kwa bao 1-0 kama siyo shuti la
Ismail Dunga kukosa shabaha akiwa na kipa Ally Mustapha baada ya
kuipangua ngome ya Jangwani alivyotaka.
Dunga alimjaribu tena Mustapha kwa shuti nje ya 18
katika goli la Jangwani, lakini kama ilivyokuwa awali, shuti lake
lilipotea njia na kutoka nje dakika ya 20.
Kocha Ernest Brandts aliwapa nafasi chipukizi
wawili kutoka kikosi B cha Yanga, George Banda na Rehani Kibingu kuvaa
kwa mara ya kwanza jezi za kikosi A sawa na usajili mpya, Kabange Twite.
Pacha wa Kabange, Mbuyu Twite na Hamis Kiiza walianza benchi katika mchezo huo, ambao ilishuhudia kipindi cha kwanza kikosa ushindi kutoka pande zote mbili.
Pacha wa Kabange, Mbuyu Twite na Hamis Kiiza walianza benchi katika mchezo huo, ambao ilishuhudia kipindi cha kwanza kikosa ushindi kutoka pande zote mbili.
Yanga walitumia mfumo wa kugongeana pasi fupi,
huku wapinzani wao wakicheza pasi ndefu na kujipatia bao la kuongoza
likifungwa na Dunga kwa kiki ya penalti baada ya Nurdin Bakari
kumwangusha Khalid Aucho.
Kipindi cha pili, Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa, Banda, Rehani, Ladislaus Mbogo na OscarJoshua na kuwaingiza, Stephano Mwasika, Omega Same, Kiiza na Simon Msuva.
Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuisaidia sana Yanga, kwani waliendelea kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mbele ya mashabiki wake wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuisaidia sana Yanga, kwani waliendelea kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mbele ya mashabiki wake wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Tusker waliokuwa wakicheza vizuri na kuonana kwa
pasi ndefu, walikaribia kufunga katika dakika ya 54 kama siyo juhudi ya
Mustapha kuicheza kiki kali ya Michael Olunga.
Yanga waliibuka dakika 20 za mwisho kwa kupiga kambi kwenye lango la Tusker iliyokuwa na beki imara na kuwabana vilivyo washambuliaji wa Yanga.
Yanga waliibuka dakika 20 za mwisho kwa kupiga kambi kwenye lango la Tusker iliyokuwa na beki imara na kuwabana vilivyo washambuliaji wa Yanga.
Kikosi cha Brandts kingeweza kupata bao la
kusawazisha kama jitihada za David Luhende zisingeishia kuupeleka mpira
nje baada ya kupiga krosi fyongo.
Kiiza naye aliinyima Yanga bao katika dakika ya 65 baada ya shuti lake kali kwenda nje ya lango la Tusker. SOURCE: MWANANACHI.
0 comments:
Post a Comment