Tatizo la maji katika vijiji
vingi vya Tanzania limezidi kuwa kero na sugu, na kuwafanya wakazi wengi wa
vijiji hivyo ama kupata maji mbali au kupata maji ya matumizi yao ya kila siku
kama kunywa, kufulia, kupikia na kuogea katika vyanzo ambavyo vinatoa maji
ambayo si safi wala salama.
Pichani ni wakazi wa Kijiji cha
Samaria kilichopo Wilayani Arumeru mkoani Arusha wakisafiri umbali mrefu
kwenda kutafuta maji wakiwa na Wanyama kazi wao (Punda) ambao huwasaidia kubeba
madumu hayo.
Wakazi hao wa Kijiji cha Samaria
ambacho kinakaliwa zaidi na jamii ya wafugaji hulazimika kutoka kijijini hapo
hadi jirani na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwaajili ya
kupta maji safi ya kunywa na kupikia.
Serikali haina budi kuwasogegezea
wakazi hao huduma ya maji safi Kijijini Samaria ili kuwapa fursa wakazi hao
kufaidi Matunda ya Uhuru na pia kuwaokolea muda mwingi wanao poteza hasa akina
mama na watoto wa kwenda kusaka maji na kushindwa kufanya shughuli nyingine za
kijamii katika familia.
Wasichana wadogo wa jamii za wafugaji kutoka Kijiji cha Samaria wakiswaga punda wao kuelekea eneo lenye maji jirani na Uwanja wa Ndege wa KIA.
Nimisafara mirefu ya Punda kutoka Kijiji cha Samaria huonekana ikiwa imebeba madumu ya maji.
0 comments:
Post a Comment