Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, akizungumza na
waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza udhamini wa kampuni hiyo katika Mbio
za Kili Marathon kwa Mwaka huu, Vodacom imedhamini Mbio za kilomita 5 za Fun
run ikiwa ni Mara ya sita mfurulizo. Pamoja nae ni Mratibu wa mashindano hayo
Angela Damas.
*******
Vodacom yadhamini mbio za Vodacom 5km Fun Run kwa mara ya sita
10/12/2012 Kwa
mara nyingine tena Vodacom Tanzania inadhamini mbio za kujifurahisha za
Vodacom 5km Fun Run ambazo ni sehemu ya mbio za Kilimanjaro Marathon
zinatarajiwa kufanyika tarehe 3 Machi 2013 huko Moshi. Hii ni mara ya
sita kwa Vodacom kudhamini mbio hizi.
Akiongea
na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutangaza uzinduzi huo, Mkuu wa
Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema: “Tumeamua kudhamini tukio
hili kwa sababu linawaleta pamoja watu kutoka nyanja mbalimbali katika
maisha.
Vodacom
5km Fun Run ipo kwa ajili ya kutoa fursa kwa watu wa umri na makundi
mbalimbali kushiriki katika mbio hizi za kimataifa na kuzidi kuifanya
Kilimanjaro Marathon kuwa tukio linalohusisha watu wote.”
“Tuna
shauku kubwa kuweza kuwa sehemu ya Kilimanjaro Marathon tukio ambalo
hivi sasa ni kati ya matukio makubwa kabisa ya kimichezo hapa Tanzania
na katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Tukio
hili linavutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.
Vilevile ni muhimu kusema kwamba tukio hili limeweza kuvuta hisia za
wapenzi wa mbio ndefu duniani”.
Tangu
tulivyodhamini tukio hili kwa mara ya kwanza mwaka 2008, tumeshuhudia
mbio hizi zikikua kwa kasi ya aina yake na tumefurahishwa na fursa ya
kuendelea kuwa sehemu ya Kilimanjaro Marathon ambapo tuna nafasi ya
kuwaunga mkono wanariadha wetu katika tukio hili la kimataifa
kimichezo,” aliongeza.
Vodacom
itahakikisha kuwa kila mtu anakuwa sehemu ya shamrashamra za siku hiyo
kwani maana itatoa fursa kwa wanaotaka kutembea, kukimbia na hata
kutambaa kila mmoja kwa mwendo wake kushiriki.
Mbali
na udhamini wa mbio hizo za kujifurahisha, Vodacom pia itahakikisha
waandaaji wa mbio hizo wanakuwa na mawasiliano ya uhakika kwa kuwapa
namba maalum za simu pamoja na muda wa maongezi.
Ikiwa
ni sehemu ya ushiriki wetu kwenye Kilimanjaro Marathon, tutaleta
wafanyakazi wetu kushiriki kwenye Kilimanjaro Marathon Corporate
Challenge na vilevile taasisi yetu ya Vodacom Foundation itatumia tukio
hilo kusaidia jamii katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa sababu tunaamini
katika kuleta mabadiliko na kuboresha maisha ya Watanzania wote.
0 comments:
Post a Comment