Ukiangalia
katika picha hii utawakumbuka watoto hawa Nyambuli Mganga (5) na
Gozbert Bwere (3) kutoka mkoani Mara ambao walikuja jijini Dar es salaam
na kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani humo, kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kwenye
uwanja wa Uhuru, watoto hawa walitia fora sana mbele ya Amiri Jeshi Mkuu
na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na wageni
mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi waliohudhuria katika maadhimisho
hayo.
Shughuli
kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa
ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali
kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC
CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba
walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.
Katika pita pita za kusaka habari maeneo ya Manzese katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds
Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli
hiyo, akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni msaidizi wa
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na
kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.
Chakusikitisha
sana ni kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa inayodhaniwa kuwa na pombe kali akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko , huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kilevi.
Kitu
kilichiniumiza sana nilipoongea na Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa
wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma. Hivyo watoto hao wako chini ya
uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano
mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa
kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe na kiongozi huyo.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama
hicho Mwigulu Nchemba wakirejea jukwaani mara baada ya kuwatunza watoto
hao Nyambuli na Gozbert wakati wakicheza ngoma katika maadhimisho ya
miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akionyesha uwezo wake katika kupiga ngoma huku akiwa amelala chini katika maadhimisho hayo.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akifanya vitu vyake katika kupiga ngoma katika maadhimisho hayo. (Na FULLSHANGWEBLOG.COM)
0 comments:
Post a Comment