Nafasi Ya Matangazo

December 10, 2012

Nahodha wa Mabingwa wa Soka bara Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, Christopher Katongo (pichani), anataraji  kukiongoza kikosi chaeke kupambana na kikosi cha Juma Kaseja Taifa Stars Desemba 22, mwaka huu katika nyasi za Uwanja wa taifa.

Kocha Mkuu wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.

Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Posted by MROKI On Monday, December 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo