Marwa
Tawfik (Kulia) mmoja wa wajumbe waliowakilisha vyombo vya habari nchini
Misri kuja Tanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii akifafanua
jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya kile walichojionea walipofanya ziara
katika vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Zanzibar.Wengine
ni baadhi ya wawakilishi kutoka Misri.
********
Na Mwandishi Wetu
VYOMBO
vya habari nchini Misri vimeahidi kutangaza vivutio mbalimbali vya
utalii vilivyopo nchini katika kuhakikisha Tanzania inapata watalii
wengi zaidi jambo litakaloendelea kudumisha mahusiano mema yaliyopo kati
ya nchi hizo.
Hayo
yalisema Dar es Salaam juzi na mmoja wa wawakilishi wa vyombo vya habari
nchini Misri, Marwa Tawfik alipozungumzia ziara waliyofanya katika
vivutio vya utalii nchini ambapo waliahidi kutumia vyombo vyao kutangaza
walivyoviona.
Ujumbe
wa watu sita uliowakilisha vyombo mbalimbali vya habari nchini Misri
yakiwemo magazeti na televisheni chini ya Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania
nchini humo Jestas Nyamanga walifanya ziara ya siku tano nchini
kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Visiwani chini
ya uratibu wa Bodi ya Utalii nchini (TTB).
Alisema
wanaporudi nchini kwao watakaa na uongozi wa vyombo vyao na kuangalia
jinsi ya kupata vipindi maalumu katika televisheni na makala katika
magazeti jambo litakalowezesha taarifa za utalii za Tanzania kuwafikia
watu wengi zaidi nchini mwao na nchi nyingine za ukanda huo.
Tawfik
alisema ana imani ziara hiyo pamoja na kazi watakayoifanya ya
kuvitangaza vivutio husika itasaidia Tanzania kupata watalii wengi zaidi
kutoka nchini mwao na katika nchi za ukanda wa kiarabu. “Tumeona
utajiri wa asili wa ajabu uliopo Tanzania,sisi tunaahidi kutumia vyombo
vyetu kutangaza vivutio hivi katika kuhakikisha watu wengi zaidi
wanahamasika kuja Tanzania na hatimaye kuwaongezea pato lenu kupitia
utalii,” alisema Tawfik.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Aloyce Nzuki alisema ziara hiyo
pamoja na nyingine ni muendelezo wa jitihada za bodi hiyo ya kuhakikisha
sekta ya utalii inakua ndani na nje ya nchi.
Alisema
ujio wa ujumbe huo kutoka Misri utaongeza idadi ya watalii kutoka nchi
hiyo pamoja na nyingize za ukanda huo ambapo takwimu za sasa zinaonyesha
Tanzania inapata watalii 25,000 kutoka nchi za ukanda huo.
Nzuki
alisema pamoja na ujumbe huo kuahidi kutumia vyombo vyao kutangaza
walivyoviona pia bodi hiyo inaendelea na jitihada za kuhakikisha
matangazo ya vivutio vilivyopo nchini yanawekwa katika lugha ya
Kiswahili katika kukuza utalii wa ndani.
“Tumekuwa
na jitihada endelevu za kuhakikisha vivutio tulivyonavyo vinajulikana
ulimwenguni kote jambo litakalosaidia kupata watalii wengi zaidi kutoka
nje lakini pia tunaendelea na jitihada za kuhakikisha utalii wa ndani
unakua,” alisema Nzuki.
0 comments:
Post a Comment