Nafasi Ya Matangazo

November 03, 2012

Vyakula bahari vya aina mbalimbali vinavyopatikana katika eneo la bustani ya Forodhani katika kisiwa cha Unguja mjini Zanzibar. Bustani hii imejizolea umaarufu mkubwa si kwa watu tu kupumzika nyakati za mchana bali pia kwa uuzaji huo wa vyakula nyakati za usiku ambapo hutapakaa meza mbalimbali za kuuza minofu ya samaki, Pweza, Ngisi, kuku na mishkaki ya Ng'ombe sambamba na chips mayai na ndizi za kukaanga. Hakika ukifika Zanzibar na ukapata wasaa wa usiku mmoja kukuta katika kisiwa hicho hupaswi kuacha kufika enehilo ambalo kando yake kuna eneo maarufu la Ngome Kongwe na Makumbusho ya Taifa.
Posted by MROKI On Saturday, November 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo