Wizara ya Nishati na Madini imeandaa ziara ya mafunzo kwa waandishi wa
habari katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuwapa fursa ya kujionea na
kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo.
Msemaji wa Wizara, Bw Fadhil Kilewo amesema waandishi wanaoshiriki katika
ziara hiyo watasaidia kufikisha taarifa kwa watanzania kuhusu shughuli na
huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara yake katika Kanda ya Kusini.
Aidha, Bw Kilewo ameongeza kuwa waandishi hao pia watapata fursa ya
kuzungumza na wananchi katika maeneo husika kusikia maoni yao juu ya huduma
zitolewazo na wizara hali itakayowawezesha kutoa taarifa sahihi kwa pande zote
mbili yaani serikali na wananchi kupitia vyombo vya habari.
Ziara hiyo ya siku kumi ilianza tarehe moja mwezi huu wa Oktoba, ikiwa ni mwendelezo
wa mikakati mahsusi na endelevu ya wizara kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu
kazi inazofanya na pia kusikia maoni kutoka kwa wananchi ili kuboresha utendaji
wake.
Waandishi
wa habari wakifanya mahojiano na Kaimu Meneja wa Tanesco wa Mkoa wa Mtwara, Bw
Daniel Kiando kuhusiana na mradi wa umeme wa uhakika vijijini unaozalishwa kwa
kutumia gesi asilia. Hapa ni Kijiji cha Mbambakofi, Mtwara Vijijini.
Mkazi
wa Kijiji cha Mbambakofi, Mtwara Vijijini, Aisha Laisi (Mwenye ushungi) akitoa
maoni yake kwa waandishi wa habari. Bibi Aisha amesema amefarijika sana na
punguzo la kuunganishiwa umeme lililotolewa na Serikali kwa Vijiji vya Lindi na
Mtwara.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mtwara, Bw
Daniel Kiando akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mbambakofi na kuwasisitiza
watumie fursa ya punguzo la umeme iliyotolewa na Serikali kuunganisha umeme
katika makazi yao kabla ya muda uliotolewa kuisha.
Transfoma
yenye uwezo wa kubeba umeme wa Kilovolti 25 katika Kijiji cha Mbambakofi. Kwa
mujibu wa Meneja Kiando, kiasi hicho cha umeme ndicho kinachohitajika kwa
matumizi ya kijiji hiki.
Mkazi
wa Kijiji cha Mbambakofi, Hamidu Selemani akiwa nje ya nyumba yake. Bw Selemani
amekamilisha taratibu zote za kufungiwa umeme na ni miongoni mwa wakazi
watakaonufaika na punguzo la gharama za kuunganishiwa umeme.
Nyumba
ya mkazi wa Kijiji cha Nanyamba Wilaya ya Tandahimba iliyonufaika na Mradi wa
Umeme Vijijini. Nyumba hii inatumia mita ya Luku.
Kazi
ya kusimika nguzo ikiendelea katika moja ya vijiji vitakavyonufaika na Mradi wa
Umeme Vijijini.
Msemaji
wa Wizara, Bw Fadhil Kilewo akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa waandishi
wa habari katika ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment