Mkurugenzi
Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akiongea na waandishi wa habari
(Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa
uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za
kununua chakula chenye lishe. Walengwa watakuwa wakipokea fedha kila
mwezi kupitia mtandao wa M-PESA. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom
Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkurugenzi
Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikakati)akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa
uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za
kununua chakula chenye lishe. Walengwa watapokea fedha hizo kupitia
huduma ya M-pesa. Wengine pichani ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom
Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Ofisa lishe wa WFP Rosemary
Mwaisaka.
Mkuu wa
kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto)
akiteta jambo na Mkurugenzi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan,wakati wa
mkutano na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa Vodacom Tanzania na
WFP katika mradi wa uwezeshaji wanawake wajawazito fedha za kununulia
chakula chenye lihse mkoni Mtwara. Feha hizo hutumwa kupitia huduma ya
M-pesa.
*****
DAR ES
SALAAM - Vodacom Tanzania na Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP)
leo wametangaza ushirikiano ambao utahamasisha jamii zisizokuwa na
uhakika wa chakula katika Mkoa wa Mtwara kupata elimu ya afya na lishe
na kwa njia ya kupatiwa msaada wa fedha kupitia mtandao wa simu za
mkononi.
Mradi huu
wa majaribio, ambao utazinduliwa Jumanne 9 Oktoba 2012 katika Kata ya
Nanguruwe, Mtwara, utakuza desturi chanya za lishe kwa njia ya kutuma
fedha kwa kutumia Vodacom M-Pesa. Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye
tatizo sugu la utapiamlo na ukosekanaji wa virutubishi muhimu kwa muda
mrefu.
Mkurugenzi
wa WFP Nchini, bwana Richard Ragan, alisema ushirikiano huo na Vodacom
utasaidia kufikisha elimu ya lishe kwa kaaya zilizolengwa zipatazo
2,200 katika sehemu zote za mkoa wa Mtwara kwa kutoa motisha kwa kina
mama kushiriki kwenye mafunzo.
"Teknolojia
ya simu za mkononi ya M-Pesa inatoa njia mbadala ya usambazaji wa
chakula," alisema Ragan." Kwa kusaidiana na Vodacom Tanzania, WFP
inachangia juhudi za kitaifa za kupambana na lishe duni hapa Tanzania."
Akina
mama watakaoshiriki watatumiwa kwa M-Pesa kiasi cha TShs 16,000
(takriban dola za kimarekani 10) kila mwezi , ambazo zitawawezesha
kununua chakula kinachojenga afya zaidi na chenye virutubisho zaidi.
Fedha hizi zitatumwa kutegemeana na mahudhurio kwenye kliniki za
kuelimisha kuhusu umuhimu wa lishe kwa mtoto "Katika Siku Zake Elfu Moja
za Kwanza " za maisha ya mtoto, ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Vodacom Foundation Bwana Yessaya
Mwakifulefule alisema Vodacom Tanzania itaendelea kuisaidia miradi ya
Vodacom Mobile for Good, inayoboresha maisha ya vikundi vilivyo hatarini
hapa nchini kwa kulenga maeneo muhimu ya afya na ustawi wa jamii.
"Kupitia
Vodacom M-Pesa, tutaisaidia WFP kutuma pesa kila mwezi moja kwa moja kwa
walengwa stahili. Hii, pamoja na elimu ya lishe, itawahamasisha akina
mama walio wajawazito na wanaolea watoto wachanga na akina mama wenye
watoto walio chini ya miaka 2 kununua chakula kinachojenga afya na
kuifanya milo yao iwe anuwai," alisema Mwakifulefule.
"Vodacom
Tanzania ina furaha kuwa sehemu ya mradi huu kabambe; ni lengo la
kampuni kuhakikisha teknolojia yake ya simu za mkononi inabadili maisha
ya watu katika kila sekta nchini," aliongezea. Mradi utafanyiwa majaribio katika vijiji 27 katika kata za Nanguruwe, Naumbu, Madimba na Nitekela,
zilizoteuliwa
kwa kushauriana na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Huu ni mradi wa
kwanza wa kulipa fedha taslimu ambao WFP iaufanyia majaribio Tanzania,
na utapima jinsi malipo ya pesa taslimu yanavyoweza kufanyika katika
miradi ya jamii inayowalenga mama na mwana katika masuala ya, na
shughuli za, lishe.
0 comments:
Post a Comment