Viongozi mbalimbali waliokusanyika hapa Umoja wa Mataifa katika
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ambayo kwa mara ya
kwanza imefanyika hapa Umoja wa Mataifa. Mwezi Desemba mwaka jana Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio lililotamka kwamba Octoba 11
ya kila mwaka itakuwa ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike
Pichani ni watoto wakike wakiwa katika sare zao za shule, Umoja wa
Mataifa umeitenga Octoba 11 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataaifa ya
Mtoto wa kike, madhumuni yakiwa ni pamoja na mambo mengine kutathimini
changamoto za msingi zinazomkabili mtoto wa kike kama vile ndoa za
utotoni. Maadhisho ya mwaka huu ambayo yamefanyika siku ya Alhamisi
yaliambatana na majadiliano yaliyowahusisha watu mashuhuri akiwamo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon na Askofu Mkuu Desmond Tutu.
Ujumbe maalum wa mwaka huu katika maadhimisho hayo ulikuwa " Ukomeshaji
wa Ndoa za Utotoni".
0 comments:
Post a Comment