NI KATIKA KUHITIMISHA KILELE CHA MSIMU WA SERENGETI FIESTA 2012.
Lile
tamasha kubwa kuliko yote hapa nchini, maarufu kama Serengeti Fiesta
ambalo limekuwa likizunguka mikoa ya Tanzania bara na kufika takribani
mikoa 11 sasa linaelekea katika kilele chake katika viwanja vya Leaders
Club jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi wiki hii ambapo msanii wa
hiphop kutoka nchini Marekani Leonard Roberts maarufu kama Rick Ross
atatumbuiza katika tamasha hilo.
Akizungumzia
ujio wa msanii mkubwa kama huyo katika mahojiano maalum jijini Dar es
Salaam leo, Meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo amesema tamasha
la Serengeti Fiesta limekuwa likifanya vizuri sana katika mzunguko wake
na kwamba watanzania wamekuwa wakifurahia uwepo wa tamasha hilo kutokana
na mafanikio mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyapata kila ilipofika msimu
wa Serengeti Fiesta “mwaka huu tutakuwa na Rick Ross na kwamba
watanzania waendelee kujenga imani na Kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager, kwani kila kilele cha msimu
wa tamasha hili ndio mwanzo wa maandalizi ya msimu unaofuata”.
Rick Ross
ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaotamba sana katika miondoko ya
kurap (hip hop) nchini marekani, atawasili hapa nchini siku ya alhamisi
tayari kabisa kutumbuiza katika maadhimisho ya kilele cha tamasha la
Serengeti Fiesta siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki hii.
Msimu wa
Serengeti fiesta ulianzia katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Musoma,
Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Iringa
ambapo wakazi wake walipata burudani na ladha ileile ya bia ya Serengeti
kabla ya kufikia mwisho wa msimu wake wiki hii. Wasanii
waliburudisha katika tamasha la Serengeti Fiesta nyanda za juu kusini
ni pamoja na Inspector Haroun, Juma Nature, Roma Mkatoliki, Linah,
Amini, Supa nyota Serengeti fiesta 2012 na wengine.
Maelfu ya
wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani wanatarijwa
kumiminika katika viwanja vya Leaders Club kushuhudia burudani
mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa hapa nchini, kabla ya kilele cha
msimu wa ‘BHAAAS’ kumaliziwa na msanii Rick Ross na kundi lake kwa
kiingilo cha shilingi 20,000/= za kitanzania kwa wale watakaonunua
tiketi zao mapema na elfu 25,000/= kwa wale watakaonunu tiketi getini.
Katika
tamasha la Serengeti Fiesta msimu wa uliopita uliokuwa ukijulikana kama
‘Haina Majotroo’ Kampuni ya bia ya Serengeti iliwaleta wasanii maarufu
ambapo msanii wa muziki wa raga ‘Shaggy’ alitumbuiza katika uzinduzi wa
msimu huo jijini Mwanza na msanii nyota kutoka nchini Marekani Ludacris
alihitimisha msimu wa kwa kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar Es Salaam
na majirani zake kama kawaida katika viwanja vya Leaders Club.
Umaarufu
wa tamasha Serengeti Fiesta umekuwa ukitengeneza ajira mbalimbali za
muda mfupi na kudumu, na pia nyingine zikianzishwa kupitia Serengeti
Fiesta katika maeneo yote ambayo tamasha hilo lilipata kupita zikiwemo
kuibuliwa kwa wasanii chipukizi na baadaye kujitegemea kimuziki,
kujengeka kwa majina ya wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika
zaidi kwa mashabiki wa muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu
kupitia tamasha hili la Serengeti Fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya
bia ya Serengeti kupitia bia ya Serengeti Premium Lager.
0 comments:
Post a Comment