Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) imezindua
ofisi mpya katika kata ya Usariver wilayani Arumeru ikiwa ni moja kati ya
kuboresha huduma za wanachama wake katika wilaya hiyo ili kuweza kuwasogezea
huduma wananchi karibu zaidi.
Akizungumza katika uzinduzi huo
mkurugenzi mtendaji wa NSSF , Ramadhani Dau amesema kuwa wilaya hiyo ni moja
kati ya wilaya ambazo zinaiingizia michango mingi zaidi katuika mfuko huo
ambapo amesema kuwa mwezi huingiza milioni 432 kwa mwezi.
Bw.Dau aliongeza kuwa mchango huo kwa
mwezi ni mkubwa sana kwa kuwa ndani ya mwaka mzima ni sawa na shilingi biloni
tano hali mbayo inaashiria kuwa kukiwa na ofisi hiyo karibu kutaongeza idadi ya
wananchama wengine wapya katika mfuko huo.
“mfuko wa hifadhi ya jamii umeona ni
vyema kama watatumia njia nzuri kuwa karibu na wananchama wake kwa kuweka ofisi
hii nyinyi ili kuwapunguzia bughudha ya kufuatilia mafao pamoja na kuweka
michango yenu hivyo nadhani hii itawasidia sana”alisema bw.Dau
Aidha alifafanua kuwa lengo la nssf
kufungua ofisi hiyo ni ili kuwa karibu na wananchama ili waweze kuweka michango
yao kwa urahisi zaidi na kuwapunguzia gharama za kufuatilia mafao wanachama
ambapo ahapo awali walikuwa wanalazimika kufuata huduma zote za mfuko mjini
Arusha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji
bw.Cricentus Magori alisema kuwa shughuli ambazo zinafanyika katika wilaya hiyo
haswa mashamba makubwa ya maua ambayo yapo maeneo mbalimbali,shughuli za
uchimbaji wa madini ndio chachu ya kupata michango mingi ,na wnachama wengi
katika wilaya ya arumeru.
Bw.Magori alisema kuwa kwa sasa wilaya
hiyo ina wanachama elfu saba ambapo alisema kuwa wameona ni muhimu kufungua
ofisi ili kuwapatia huduma na kuondoa usumbufu wa kufuata huduma hizo mjini
Arusha.
Katika uzinguzi huo uliofana sana
ulifanyika katika kata ya usa river wilayanu arusmeru na kuwashirikisha
wafanyakazi na wanachama wa mfuko huo pamoja na wadau mbalimbali
0 comments:
Post a Comment