Wafanyakazi
wa Airtel wakiwa na balozi wao Ambwene Yesaya katika picha ya pamoja
na wanafunzi wa shule ya sinza Maalum iliyopo jijini Dar Es Salaam
walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii kama mwendelezo wao wa
kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wao wa
kuchangia Elimu kwa kushirikiana na BAMVITA.
Mwananafunzi
wa shule ya Sinza Maalum akiimba wimbo wa mwanamuzi Ambwene Yesaya (AY)
walipotembelewa na mwanamuzi huyo mwishoni mwa wiki hii wakiongozana na
wafanyakazi wa Airtel, kushoto ni meneja mahusiano wa jamii wa Airtel
Hawa Bayumi, watatu kutoka kulia Ambwene Yessaya (AY) akifwatiwa na
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.
Balozi wa
Airtel Ambwene Yesaya (AY) wakiimba kwa pamoja na mwanafunzi wa shule
ya Sinza Maalum (Kushoto) mwishoni mwa wiki hii walipotembelewa na
mwanamuzi huyu aliyeongozana na wafanyakazi wa Airtel kama mwendelezo
wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wao
wakishirikiana na Bamvita wa kuchangia Elimu.
********
Na Mwandishi wetu.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii
imeanza mchakato wa kutembelea baadhi ya shule zitakazonufaika na mradi
maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea
changamoto zinazowakabili pamoja na kuwahimiza watanzania kuweza
kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la maendeleo
ya vitabu Tanzania (BAMVITA).
Afisa
mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo
ikiwa na Balozi wake msanii Maarufu AY itatembelea shule zote zilizopo
Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubaiunisha matatizo wanaoyokumbana
nayo ili kuona namna ya kuwasaidia. Amesema shule za wanafunzi wenye
mahitaji maalum zinahitaji vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi
hao kuweza kupatiwa elimu inayostahili.
“Shule
hizi zinamahitaji mengi sana, Airtel tumeona ni vyema kumtumia pia
Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y kuendea kuwafikishia jamiii
ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu wenye lengo la kuendeleza
jamii” alisema Bi DANGIO KANIKI Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel
Akizungumza
mara baada ya kutembelea shule ya msingi Sinza Maalum Balozi wa Airtel
AMBWENE YESAYA (A.Y) amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia
kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
“Watoto
hawa wenye uhitaji maalum nimejionea mwenyewe kuwa wakiwezeshwa
wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi kushirikiana na Airtel pamoja
na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunawachangia vijana wetu hawa nao
waweze kuendeleza hata vipaji vyao pamoja na elimu yao .
Ninaomba
kuwakubusha watanzania kuchangia katika kuwapatia vijana hawa vifaa
mbalimbali ambavyo ni changamoto kwao, unaweza kuchangia kwa kupitia
Airtel Money ambapo unaandika jina la fumbo VITABU na utatuma kiasi
chochote au kwa kutuma SMS yenye neno VITABU kwenda namba 15626 na
atakuwa amechangia shilingi 200 tu.
Watanzania
naomba tusaidiane katika elimu kwa kuwa tuanaamini Tanzania itajengwa
na sisi wenyewe. Alimalizia kusema AMBWENE YESAYA ---Balozi wa Airtel
.Wakati wa ziara hio mwuishoni mwa wiki hii Mwalimu Mkuu wa shule ya
Sinza Maalum, SIMON Milobo alibainisha kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia pamoja na
mafuta ya kuendeshea gari la wanafunzi.
Kampeni
ya Airtel kwa kushirikiana na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi
mitatu , na Watanzania wataweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu”
kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa
umechangia shilingi 200 itakayoingizwa katika mradi huu”
0 comments:
Post a Comment