Kocha wa Yanga Tom Santfiet akionekana pichani akikuna kichwa. Kocha huyu wa Kigeni kutoka nchini Ubelgiji ambaye aliisaidia Yanga kutwaa Kombe la Kagame na kushinda mechi kadhaa za kirafiki lakini ameshindwa kuonesha makali yake katika mechi mbili za awali za ligi kuu ya soka Tanzania bara anadaiwa kutimuliwa katika timu hiyo.
Taarifa za ndani zinadai kuwa Kocha huyo ametimuliwa baada ya kutokea hali ya kutokubaliana mambo na waajiri wake hasa tabia yake ya kuzungumza hovyo mambo ya ndani ya timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment