Mkurugenzi
wa mahusiano na Sheria wa kampuni ya Bia TBL,Stephen Kilindo(kulia) akimkabidhi
mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 51.6 mkurugenzi wa kampuni ya Dr
Gogo Engeneering Cmpany Ltd,Bw
Godwin Kallaghe(mwenye kofia) kwa ajili ya shughuli ya uchimbaji wa kisima
chene urefu wa futi 120 katika kata ya Makanya wilayani Same.
Wananchi
katika kata ya Makanaya wilayani Same wakishuhudia zoezi la utolewaji wa hundi
ya kiasi cha shilingi milioni 51.6 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha
maji.Hundi hiyo imetolewa na kampuni ya Bia Tanzania TBL.
Wananchi
pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa TBL, wakianya sara katika eneo ambalo
kisima chenye urefu wa futi 120 kinachimbwa mara baada ya TBL kutoa kiasi cha
shilingi milioni 51.6 kwa ajili ya shghuli za uchimbaji huo.
Waziri
wa miugo na uvuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dk Mathayo
David akizungumza na wananchi katika eneo la Makanya ambako kisima chenye urefu
wa futi 120 kinachochimbwa kwa msaada wa kampuni ya Bia Tanzania TBL ambao
wametoa kiasi cha shilingi milioni
51.6 kwa ajili a shughuli hiyo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Dr Gogo Engeneering Cmpany Ltd,Bw Godwin Kallaghe akizungumza na wananchi
(hawapo pichani)mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi,Kallaghe amesema zoezi
la uchimbaji wa kisima hicho utafanyika kwa muda wa wiki tatu hadi kukamilika
kwake.
0 comments:
Post a Comment