Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea nakala ya machapisho mbalimbali ya Bunge la Afrika Mashariki toka kwa Spika wa Bunge hilo Bi. Margaret Banbtonbg Zziwa alipomtembelea Ikulu Jumatano Septemba 19, 2012.
**************
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amelishauri Bunge la Afrika Mashariki (EAC) kuzingatia na
kufuata maelekezo yaliyomo kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo wakati wa
kuwasilisha na kujadili hoja zao.
Rais
Kikwete ametoa ushauri huo jana jioni (19 Septemba, 2012) alipokutana na Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Margareth Ziwa, Ikulu.
“Jumuiya
ya Afrika Mashariki inahusika na masulala yaliyomo kwenye Mkataba (Treaty) na
Itifaki zilizoanzisha Jumuiya hii na kila nchi inawajibu wa kuzingatia
kilichomo kwenye Mkataba” ameeleza na
kufafanua “Lakini pia msisahau kuwa hizi ni nchi huru zenye sheria na taratibu
zake ambazo nchi zinapaswa kuzifuata na kuzizingatia, hivyo Bunge la Afrika
Mashariki linaweza tu kuzishauri lakini sio kuzielekeza au kuzilazimisha
kutekeleza jambo ambalo halimo kwenye Mkataba ambao nchi hizi zimetiliana
saini” ameongeza.
Mheshimiwa
Ziwa amefika Ikulu kujitambulisha kwa Mheshimiwa Rais baada ya kushika wadhifa
huo hivi karibuni.
Mheshimiwa
Ziwa ni raia wa Uganda na ni Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inajumuisha nchi za Burundi, Kenya, Rwanda,
Uganda na Tanzania.
Rais
amewataka wabunge wapya kusoma Mkataba na Itifaki zilizoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ili
waweze kutekeleza majukumu yao vizuri bila kuingilia uhuru na taratibu za nchi
wanachama.
“Jipeni
muda wa kutosha wa kusoma na kuzielewa taratibu za Mkataba na Itifaki
iliyoanzisha Jumuiya hii, hii itawasaidia sana katika kujenga hoja zenu na
jinsi ya kuziwasilisha” amewakumbusha kuwa hiyo ndiyo
njia pekee ambayo itawafanya kutekeleza kazi na wajibu wao kwa umakini na uangalifu
bila kuingilia taratibu za mabunge ya nchi wanachama.
Wakati
huo huo, leo asubuhi (20 Septemba, 2012)
Rais amekutana na Katibu Mkuu wa EAC
Dkt. Richard Sezibera ambaye amefika kumueleza Rais juu ya maendeleo na
ratiba ya shughuli muhimu za Jumuiya
hiyo ambazo EAC inatarajia kuzifanya kabla ya mwisho wa Mwaka.
Rais
amempongeza Dkt. Sezibera kwa maendeleo ya Jumuiya hiyo na jinsi shughuli za
utekelezaji zinavyokwenda kulingana na ratiba ya EAC.
0 comments:
Post a Comment