Nafasi Ya Matangazo

September 26, 2012


 
Mkurugenzi wa Free Media akizungumza wakati wa kuaga Mwili wa Agness Yamo. 
Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Katika uagwaji wa mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu, Amin. PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBERY BLOG
Kutoka kulia ni Yahaya Charahani Afisa habari wa NHC, Ibrahim bakari wa Mwananchi na Kassim Mbaruku wa jamboleo
Maofisa wa Jeshi la Polisi Usalama barabarani nao walifika kuaga mwili wa marehemu, Kulia ni Afande Zauda akifuatiwa na Afande Swai.
Ni majonzi tupu yalitawala eneo la msiba
Kutoka kushoto ni wanahabari Angela Msangi TBC, Maulid Ahmad na Angela Semaya wa HabariLEO
Heshima za mwisho
Grace Hoka Mhariri wa Bingwa akitoa heshima
bado kijana mdogo
wapo walio zirai kwa uchungu
ni vilio tupu juu ya kuondokewa na mpendwa wao Agness
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda
Wanahabari kutoka Tanzania Daima alikokuwa akifanya kazi marehemu.
waombolezaji wakiingiza Sanduku lililohifadhi mwili wa marehemu.
 
Mkurugenzi wa Free Media, Lillian Mbowe
Posted by MROKI On Wednesday, September 26, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo