Waisilamu kutoka maeneo mbali mbali ya jijini Dar es Salaam wakishiriki katika maandamano ya kuelekea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kupariwa ufumbuzi wa juu ya kamata kamata ya Jeshi la Polisi dhidi ya waisilamu waliokataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.Wameendelea na msimamo wa kupingwa kukamatwa wanaokataa kuhesabiwa Sensa.Jeshi la Polisi limekubali kuwaachia huru waislamu wote waliokamatwa.Waislamu watangaza ushindi,Wasema Bado Mkuu wa baraza la Mitihani Joyce Ndalichako ajiandae na maandamano ya namna hiyo hadi ofisini kwake na baadae Bakwata wanayotaka ifutwe. Muda huu wapo hapa Msikiti Kichangani,Magomeni wanapanga Mkakati wa kuandaa maandamano mengine.
Mabango yenye maelezo tofauti tofauti.
Maandamano yakiendelea.
Maandamabo yakiwa yamefika nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waisilamu wakiswali sala ya Laasiri, mbele ya Wizara ya mambo ya ndani wakati wakisubiri viongozi wao waliokwenda kuzungumza na jeshi la polisi ili kupata ufumbuzi wa juu ya kamata kamata ya jeshi la polisi dhidi ya waisilamu wanaokataa kuhesabiwa.
Mmoja wa Waislam akiwa amenyanyuliwa juu juu.
0 comments:
Post a Comment