Nafasi Ya Matangazo

September 15, 2012

 Meneja mkuu wa shirika la ndege la Fly 540 Francis Brown (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuyatangaza huduma mpya ya safari za anga zitakatolewa na shirika la ndege la FASTJET kwa kutumia leseni ya shirika la ndege la fly 540, kulia ni afisa mtendaji wa shirika la ndege la FASTJET bw. Ed Winter.
Afisa mtendaji wa shirika la ndege la FASTJET akiongea na waandishi wa habari  katika hafla ya kutangazwa kuanza kwa huduma za safari za anga na shirika hilo kushoto kwake ni Bw, Francis Brow General manager fly 540 tanzania.
**********
 
DAR ES SALAAM 15 SEPTEMBA 2012: Huduma za safari za ndege zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku hapa nchini ambapo jana Afisa Mtendaji wa shirika la ndege la FASTJET  Bw. Ed Winter pamoja na Bw. Brown Francis wa shirika la ndege la Fly 540 kutoa taarifa kwa waziri wa uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe kuwa shirika la ndege la FastJet linatarajia kuanza kutoa huduma za safari za anga hapa nchini kutokea jijini Dar esSalaam.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege ya kwanza aina ya A319 yenye jumla ya viti 156, itaanza kutoa huduma hiyo mwanzoni mwa mwezi wa 11 na kwamba njia zitakazoainishwa kutolea huduma zake (route map) zitatangazwa wiki chache zijazo.

Shirika la ndege la FastJet PLC ni kampuni kubwa kutoka jijini London Uingereza yenye wanahisa wakubwa kama Lonrho PLC ambao wamekuwa wakifanya biashara barani afrika kwa zaidi ya miaka 100.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ijumaa mchana Afisa Mtendaji wa shirika la ndege la FastJet Ed Winter , amesema “ FastJet itatoa huduma zenye hadhi ya kimataifa kwa garama nafuu na kwamba tunajivunia kufanya huduma za safari za anga eneo la Africa ambapo kutokana na bei zetu kuwa nafuu sana, itakuwa ni fursa pekee kwa watanzania hasa wale ambao hawakuwahi kuwa na ndoto ya kusafiri kwa ndege kuweza kupata fursa ya kusafiri kwa njia ya hii kwa kutumia ndege zetu. ”Mr. Ed Winter aliongeza kuwa kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na uchumi unaoridhisha hapa nchini na serikali imara na makini kimaendeleo.

Shirika la ndege la FastJet, kwa Afrika, litaanzia huduma zake jijini Dar esSalaam Tanzania na baadaye kufuatiwa na Nairobi Kenya.  Tayari taratibu za awali zimeshakamilika hapa nchini.   Shirika hilo la FastJet limechukua leseni ya huduma ya safari za anga ya shirika la ndege la Fly 540 Tanzania.  

Bei za fastjet zitatakuwa kuanzia hadi dola themanini za kimarekani na watakaopanga safari zao mapema na wataweza kununua tiketi hadi kuanzia dola ishirini za kimarekani.
Posted by MROKI On Saturday, September 15, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo