Washindi 16 wa promosheni ya Vuta mkwanja wakifurahi zawadi ya pesa taslimu waliyo kabidhiwa kiwandani hapo.
Meneja uzalishaji wa Bonite Bottlers Leonard Mangupili akimkabidhi mshindi Hamid Nkya mkazi wa Ngaramtoni Arusha ,kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja
Mkuu wa masoko na mauzo wa Bonite Bottlers Christopher Loiruk akimkabidhi mshindi Rahim Hashim mkazi wa Majengo Moshi, kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.
Mratibu wa mauzo wa Bonite Bottlers Boniface Mwasi akimkabidhi mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi laki moja kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.
Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda cha vinywaji baridi Bonite Bottlers,Christopher Loiruk akizungumza na wanahabari.
*******
Mwandishi Wetu ,Moshi.
KAMPUNI ya vinywaji baridi jamii ya Coca Cola ,Bonite Bottlers jana imekabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa washindi kumi na sita wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambayo inafikia tamati mwezi huu.
Washindi katika promosheni hiyo iliyoanza mwezi Julai mwaka huu ni pamoja na Fredy Charles ,Hamid Nkya wote wakazi wa Arusha na Rahim Hashim mkazi wa Majengo mjini Moshi ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Washindi wengine ni Goodluck Kessy ,Focus Njau ,Joseph Kauwedi,Samson Mushi na Fatuma Ibrahimu ambao walijishindia kaisi cha shilingi laki moja kila mmoja.
Washindi wengine ni Goodluck Kessy ,Focus Njau ,Joseph Kauwedi,Samson Mushi na Fatuma Ibrahimu ambao walijishindia kaisi cha shilingi laki moja kila mmoja.
Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda hicho Christopher Loiruk aliwataja washindi wengine waliojishindia kiasi cha shilingi lakini moja kuwa ni Julius Michael,Christina Kessy,Dorin Masawe na Khadijah Said.
Aliwataja washindi wengine ambao wamepatikana katika mikoa ya Arusha, Kilimnjaro Singida na Manyara kuwa ni Lucas Sumari ,Magdalena John na Lilian Maro ambao wote walikabidhiwa fedha zao kiwandani hapo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi ,Loiruk alitoa wito kwa wateja wa Coca cola kuendelea kunywa kinywaji hicho na jamii yake ili waweze kuibuka washindi wa zawadi mbalimbali ambazo bado zipo katika kinywaji hicho.
“Shindano promosheni imemalizika ,lakini zawadi bado zitaendelea kutolewa kwa kuwa bado zipo katika mzunguko,kuna washindi ambao wamejishindia zawadi mbalimbali kwa kunywa soda za Coca cola ,Fanta na Sprite …kila soda unayokunywa una nafasi ya kuwa mshindi”alisema Loiruk.
Alisema promosheni hiyo imewezesha wateja wengi wa bidhaa hizo kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoaja na Sh 1000,000,sh 100,000,10,000,sh 5,000 ,sh 2,000 fulana za Coca cola pamoja na soda ya bure.
0 comments:
Post a Comment