Na Ben Komba-Pwani
Kupingana na zoezi la sensa ni kupingana na amri halali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kutokana na mamlaka aliyopewa, kabla ya kuanza zoezi hilo anatakiwa kutoa Amri kama Rais ya kutangaza kufanyika kwake, muda, mahali na wahusika katika sensa.
Hayo yamesemekana katika kikao kati ya madiwani na kamati ya uratibu wa sensa Wilayani Kibaha, ambapo Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Bi. Salama Mangara amewaambia madiwani kuwa sheria hii inatamka kufuatana na sheria Namba 1 ya Mwaka 2002 kwa ajili ya zoezi la sensa ya watu na makazi kifungu cha 14.
Bi. Mangara ameongeza kuwa makosa ambayo mtu anaweza kujikuta yupo hatiani iwao atakayoyafanya ni pamoja na kumzuia Msimamizi, Mdadisi, Karani wa sensa kutekeleza majukumu yake, kukataa au kuacha kwa makusudi kujaza fomu au nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum, kukataa kujibu maswali aliyoulizwa, kutoa taarifa za uongo au kukiuka kifungu chochote cha sheria atapata adhabu ya kifungo miezi sita na faini shilingi laki 6 za kitanzania.
Bibi . Mangara amesisitiza kwa mantiki hiyo, ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake na kutoa ushirikiano unaostahili katika zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Mratibu wa sensa ya watu na makazi wilayani Kibaha, Bi. Letti Shuma akizungumza na madiwani amewataka madiwani kwenda kutengeza mazingira kwa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wao wa kushiriki kwao zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 25 na 26 mwezi huu na kuendelea kwa siku saba.
Bi. Shuma amesema malipo yote kwa wahusika wa sensa zimelipwa kiakmilifu tofauti na maeneo mengine ambayo yalikumbwa na mizozo, kilichobakia kwa sasa ni kwa wasimamizi na makarani kulipwa fedha kabla ya kuanza shughuli hiyo,zoezi ambalo limezorota kutokana na matatizo ya kibenki, lakini taarifa za uhakika ambazo anazo mpaka anapoongea na wawakilishi hao wa wananchi kua fedha hizo zimeshafika hazina tayari kwa zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment