Nafasi Ya Matangazo

August 20, 2012

Wadudu hawa wajulikanao kama Konokono kwa lugha ya Kiswahili au Snail kwa lugha ya Ulaya, ni moja kati ya vyakula vizuri sana huko nchini Liberia bara Afrika. Wadudu hawa ambao hupatikana kwa wingi pia hapa Tanzania lakini si dili zaidi ya baadhi ya watu kula konokono Bahari tofauti na hawa.


Bei ya Konokono watatu (3) ni sawa na dola (140) ya kilaiberia karibia dola 3 za Kimarekani na kwa shilingi ya kitanzania ni takribani sh.4500 hivi. Hii ni biashara ya kufanya maana hapa Bongo tunao wengi. na bei hiyo ni ya Mtaani ukiingia Super Market unaweza kukimbia.

Wanaporostiwa na kutengemnezwa vyema mchuzi wake unakuwa wa uhakika kwa kula na ugali au wali. Pichaya juu ni Konokono hao wakiwa wametoka kutafutwa katika mabonde na sehemu zilizo na maji maji.

Hivi sasa ni kipindi cha mvua nchini Liberia konokono wanapatikana kwa wingi katika kipindi cha takriban miezi 6 ambapo mvua zilianza tangu mwezi Mei
hawa ni konokono walio sindikwa na wanapatikana katika maduka makubwa "Super Market" mjini Liberia ambako huliwa kwa wingi.
Posted by MROKI On Monday, August 20, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo