Nafasi Ya Matangazo

August 24, 2012

Ni mwanzo mzuri wa mlolongo mzima wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

MOSHI, TANZANIA 22st August 2012: Lile tamasha la aina yake maarufu kama Serengeti fiesta, linang’oa nanaga rasmi siku ya ijumaa likianzia katika viwanja vya chuo cha ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka huu likiwa na kauli mbiu ‘MWONEKANO TOFAUTI BURUDANI ILEILE’.

Tamasha hilo litang’oa nanga kwa kishindo likipambwa na wasanii wakubwa wa kizazi kimpya ( Bongo flava) kama vile Juma Nature, mwana FA,  Linah,  Shettah, Rich mavoco, JohMakini, Ommy Dimpoz, Stamina,  Godzilla,Bobjr and Ferooz na wengine wengi wakipiga shoo kali huku wakimkaribisha rasmi msanii mahiri kutoka pande za Kenya mtu mzima Prezzo  maarufu kama CMB au Mr president ambaye ni siku chache tu zimepita baada ya kurudi kutoka katika shindano mahiri maarufu kama Big brother Africa lililofanyika nchini Africa ya kusini. Prezzo antaangusha burudani kali na kufanya tamasha hilo kufana sana.

Nafikiri tamasha la mwaka huu litakuwa  kubwa sana ukilinganisha na miaka iliyopita na hii inatokana  na ukweli kuwa umati mkubwa wa watu wamekuwa wakiisubiri kwa hamu na shauku kubwa sana kuliko ambavyo imezoeleka huko nyuma kwani Serengeti Fiesta 2012 itawakusanya  mashabiki kutoka pande zote za mkoa wa Kilimanjaro na wale wa mkoani Arusha huku mashabiki wengine kutoka nchi za jirani za Kenya na Uganda wakitarajiwa kufurika kwa wingi katika tamasha hilo ambalo mpaka sasa watu wamekuwa wakuwa wakinunua tiketi kwa wingi sana na kubaki hamu mshawasho wa kutaka kujua pengine nini kitajiri siku hiyo ya pekee kupata kutoke katika mji wa moshi. Hayo yalisemwa na bwana Kalinga ambaye ni mmoja wa kati mashabiki wakubwa wa tamasha la Serengeti Fiesta.

Akizungumzia Serengeti Fiesta 2012 , meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo, alikuwa na haya ya kusema, “ Serengeti Fiesta mwaka huu inakuja kwa namna ya pekee tofauti kabisa na jinsi ambavyo imezoeleka na ilivyotegewa kuwa. Mwaka huu tumekuja na zawadi mbalimbali zitakazoshindaniwa kwa kipindichote cha Fiesta, hivyo nachukua nafasi hii kuwaita wateja wetu na watanzania kwa ujumla kushiri kwa wingi katika tamasha hili na kujiuvunia kuwa sehemu ya Serengeti Fiesta mwaka huu ambapo watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Serengeti.” Alisema Chonjo .


John Maker kutoka Morogoro ,Ney Lee  kutoka Mbeyaand young Killa kutoka Mwanza, ambao wote kwa pamoja watapata fursa ya moja kwa moja kuonesha umahiri wao kwa kuangusha ngoma zao kali sambamba na wale wasanii wakubwa watakaoshiriki katika matamasha yote ya Serengeti Fiesta ambayo itaanzia Moshi mwishoni mwa wiki hii na kuelekea mikoa ya  Tanga, Musoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya, Zanzibar na baadaye fainali itafanyika katika jiji la Dar Es Salaam ambapo kutakuwa na ugeni mkubwa wa msanii maarufu wa kimataifa.

KUHUSU SERENGETI FIESTA,

Mnamo mwaka 2007, menejimenti ya PRIME TIME PROMOTIONS sambamba na CLOUDS FM waliibuka na wazo zuri la kuanzisha tamasha  la kipekee lililoitwa fiesta music concert. Baada ya mwaka mmoja tu tamasha hili lilisambaa nchi nzima na kujizolea sifa kubwa sana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania  na ndipo wazo la kuwa na tamasha la fiesta katika kila mkoa hasa katika miji mikubwa lilipozaliwa ambapo kwa mwaka wan ne sasa kampunin ya bia ya Serengeti imekuwa mdhamini mkuu wa tamasha hili kupitia bia yake ain ya Serengeti Premium Lager.

KUHUSU BIA YA SERENGETI.
Serengeti premium  Lager ni bia nzuri ilijizolea sifa maradufu kutokana na  ubora wake na ladha yake ya kipekee. Bia hii imepata kujizolea medali ya dhahabu katika ngazi ya kimataifa kama vila DLG &Monde na pia inajivunia kuwa bia ya kwanza nay a pekee kutengenezwa kwa kimea halisi kwa asilimia 100.Kwa miaka kazaa sasa kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ikitoa udhamini kupitia bia hii ya Serengeti premium Lager.Udhamini huo unajumuisha michezo kama taifa stars wakati huo na burudani kama fiesta.
Posted by MROKI On Friday, August 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo