Nafasi Ya Matangazo

August 24, 2012


JUDICA STEPHANO TERI
22.06.1946  hadi  08.03.2012
Alitwaliwa kwa amani baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marehemu Judica Stephano Teri alikuwa mume mpendwa sana wa Jane (Mwl Teri), baba mpendwa wa Joan, Linda, Davis & Hillary na kaka mpendwa wa Mony P. Sisi wote pamoja na ndugu wengine na wakwe (Aliko, Leonard & Tina), wajukuu (Tumpe, Lusako & Evan-Tumaini Alex) na marafiki wake wengi, tutamepatwa na pengo kubwa ambalo halitazibika.

Wote kwa pamoja, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kwa njia ya maombi, kadi, simu, barua pepe, michango ya hiari na kufika katika kipindi cha kuandaa na kumpumzisha mpendwa wetu Judica Teri. Tulifarijika sana kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi kwa upendo mkubwa. Tunawashukuru sana. 

Ijapokuwa tungependa tumtaje kila mmoja, lakini mtatuwia radhi kuwa sio rahisi kufanya hivyo. Tunaomba kila mmoja apokee shukrani hizi kama zake binafsi. Kipekee tunaomba kuwataja wachungaji wote kwa huduma za kiroho pamoja na ndugu wa karibu Dkt. Godbless Mlay na mkewe kwa jinsi walivyomhudumia marehemu kwa kipindi chote alipokuwa amelazwa hospitalini KCMC, Moshi. Tunawashukuru sana Ukoo wa Teri kwa maandalizi mazuri sana “aikeny mnu moose piu”, ndugu wengine, marafiki wote na wanakijiji cha Mamba Kusini kwa  kuwepo kwa wingi sana kiasi cha kufanya mazishi kuwa ya heshima kubwa. Tulifarijika sana kwa wingi wa watu wote waliofika kutoka mbali sana na karibu katika siku ya kumpumzisha mpendwa wetu Judica Teri.

MUNGU AWALINDE, AWAONGOZE KWA KILA JAMBO NA KUWABARIKI SANA! YOHANA MT. 11:25  “Yeye aniaminiye mimi (Yesu), ajapokufa, atakuwa anaishi….!
Posted by MROKI On Friday, August 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo