Nafasi Ya Matangazo

August 18, 2012

Kikosi cha timu ya Simba B ambacho kilishuka dimbani hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kumenyana na Mtibwa Suger ya turiani katika fainali za ABC Super8 Cup 2012 na kuwakimbiza wakata Miwa hao wa turiani kwa magoli 4-3. 

Simba iliwalazimu kutumia dakika 120 kuwararua wakata Miwa hao walikuwa wabishi kuwadhibiti Simba hao watoto walio kuwa wakiwatimua kila mara na mapanga yao ya kukatia miwa. 

Kwa matokeo hayo sasa Simba inakuwa timu ya kwanza kunyakua kombe hilo kwani ndio mara ya kwana kushindaniwa hapa nchini. simba pia iliwatoa Azam FC katika michuano ya Bank ABC Super8 nusu fainali kwa goli  2-1 katika mchezo huo.
Posted by MROKI On Saturday, August 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo