Nafasi Ya Matangazo

August 08, 2012

Miss Tanzania World 2012, Lisa Jensen (kushoto) akiwa na washiriki wenzake wakipita jukwaani wakati wa shindano la Mbunifu bora 'Designer Award'. 

 Miss Kenya 2012,Shamim Fauz ALI ameonekana kung’ara zaidi katika mashindano ya Miss World 2012 kwa ukanda wa Afrika Mashariki kwa kufanikiwa kuingia katika nusu fainali za mataji kadhaa yanayowaniwa katika shindano hilo kubwa la Urembo Duniani.

Miss Kenya akiwa katika kundi la tatu ametajwa kati ya warembo wanchi 40 watako wania taji la Miss Bikini ‘Beach fashion ‘ na pia yupo katika ya wasichana 47 watakao wania taji la Top Model 2012.
 Miss Tanzania akiwa katika picha hii ilipogwa katika moja ya matukio ya Miss World 2012.


Warembo watano wanaoshiriki shindano la Miss World wamefanikiwa kuingia tano bora ya shindano la Vipaji Miss World Talent  katika fainali zilizofanyika hii leo.

Warembo waliotajwa kuingia hatua ya tano bora ni kutoka nchi za Norway- Karoline OWEN, Philippines- Quenerich REHMAN,Jamaica- Deanna ROBINS, Panama- Maricely del Carmen GONZALEZ POMARES na China PR- Wenxia YU.

Mshindi wa  taji hilo atatangwzwa Jumamosi ya Agosti 18, wakati wa fainali za Miss World 2012 zitakazo fanyika katika uwanja wa Ordos Stadium Arena ambapo nchi 116 zinashiriki mashindano hayo mwaka huu. 

Onesho hilo la aina yake linataraji kushuhudiwa na watazamaji zaidi ya bilioni 1katika nchi takriban 160.  
 Miss Uganda 2012 Phiona Bizzu
Leo hii zimefanyika fainali ya Miss Talent World 2012.
Posted by MROKI On Wednesday, August 08, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo