Nafasi Ya Matangazo

August 21, 2012

Michuano ya Airtel Rising Stars barani Afrika imetimua vumbi   Jijini Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.

Michuano hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.

Michuano hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga – akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli
Michuano hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na Manchester United – zote za Uingereza.

 Kwenye uzinduzi wa michuano hiyo pia walikuwa waakilishi kutoka kwenye Klabu hizo – Mkurugenzi wa Masoko kutoka Manchester United Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka Arsenal Angus Kinnear. Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka Arsenal.

Kwenye mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi ilishinda 5- dhidi ya Kenya.

Posted by MROKI On Tuesday, August 21, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo