Na Woinde shizza Arusha
Klabu ya kijamii ya jijini arusha ijulikanayo kama kitambi noma imeandaa tamasha la idi pili amballo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kiitec uliopo kijenge jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari muheka hazina wa klabu hiyo ya KITAMBI NOMA Ayub Juma alisema kuwa tamasha hili linajumuisha watu watu mbalimbali wa marika mbalimbali na litashirikisha michezo ya aina mbalimbali.
Alitaja lengo la tamasha hili ni kusherekea kwa pamoja sikuu hii ya idi na waumini wa dini ya kiisilamu ambapo alisema kuwa katika kusherekea huko pia kutakuwa na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa.
Alitaja michezo ambayo itachezwa siku hiyo kuwa ni pamoja na kukimbiza kuku,kukimbia na makuguni ,kushindanisha watu wenye vitambi ambao ndio mchezo mkuu pamoja na mpira wa miguu ambao utawashindanisha washabiki wa timu ya yanga pamoja washabiki wa timu ya simba.
alisema pima tamasha hili litasaidia kuwaleta wanacha mwa kitambi noma na familia zao karibu na kubadilishana mawazo mbalimbali kwa pamoja pamoja na pia alisema kuwa michezo hii itasaidia kuimarisha afya kupitia michezo hii mbalimbali.
Alisema kuwa kutakuwa na zawadi kwa washindi mbalimbali ambapo alifafanua kuwa kwamshindi wa kwanza wa mpira wa miguu ataondoka na kitita cha shilingi laki 200000,na kwa upande wa michezo mingine akiondoka na shilingi 50000huku atakae kimbiza kuku atandoka na kuku wake.
Alitoa wito kwa wapenzi wa michezo mbalimbali kujitokeza kusherekea kwa pamoja kwani kiingili cha tamasha hili ni bure .
0 comments:
Post a Comment