Master J na Madam Rita wakiongea na mtoto wa mshiriki aliyetinga katika mchujo huo wa EBSS 2012 na watoto wake watatu.
Majaji wa shindano la EBSS wakila pozi la picha.
Ikiwa imeingia katika siku ya pili ya usaili wa Epiq BSS Dar-es-Salaam ambao unafanyika Coco Beach jijini hapa vijana wengi wamezidi kujitokeza kutoka maemneo mbalimbali ya jiji kusaka nafasi ya kushiki katika shindano hilo kubwa hapa nchini la kuibua vipaji vya wasanii wa muziki. Hadi jana usiku majira ya saa moja zaidi ya vijana mia tatu bado walikuwa katika foleni ya kutaka kuonana na majaji kwaajili ya usaili.
Jaji Mkuu wa Shindano la EBSS Ritta Poulsen ‘Madam Ritta’ akitafakari jambo wakati akimsikiliza mmoja wa washiriki waliojitokeza katika usaili.
Mmoja wa washiriki wa EBSS katika mchujo wa Dar es Salaam akichangia damu
Maofisa kutoka kitengo cha Damu Salama wakiendelea na shughuli ya kutoa maelezo na kupima damu kwa vijana waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa washiriki wa EBSS jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki Banana Zorro nae alikuwepo Coco Beach katika usaili wa EBSS yeye hakuwa mshiriki bali alifika kutoa sapoti kwa jopo la majaji na vijana wanaoshiriki.
Hakuna kazi rahisi hata siku moja, na hapa jamaa wakiuchapa usingizi baada ya kusubiri sana zamu yao ifike na kuweka sawa mistari yao.
Foleni ya washiriki waliokuwa wakisubiri kuonana na majaji katika usaili wa EBSS katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Coco Beach Dar es Salaam.
Hizi ni swaga za kuondokea , jamaa akitoka ndani baada ya kuonana na majaji
0 comments:
Post a Comment