Nape akihutubia baada ya kufungua kitega uchumi hiko, ambacho ni milango ya maduka 37 pamoja na kituo cha mafuta"petrol station'' mali ya CCM sumbawanga.
Kiongozi wa Kikundi cha Chipukizi wa Manispaa ya Sumbawanga Samira Samir akimfunga skafu Katibu wa Itikadi na uenezi Taifa Ndugu Nape Nnauye. Nape atakuwepo Sumbawanga kwa siku mbili katika ziara ya kuimarisha Chama.
Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi wa Manispaa ya Sumbawanga wakiwa wamesimama kikakamavu wakisubiri kumpokea katibu wa Itikadi na Uenezi ndugu Nape pamoja na Ujumbe wake wa watu Sita walio katika Ziara ya kuimarisha Chama Mkoani Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape Moses Nnauye akifungua kituo Cha Uwekezaji na kitega Uchumi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo ya Sabasaba, Manispaa ya Sumbawanga Mjini, Mkoani Rukwa Leo Tarehe 14 july 2012.
Waziri wa Maji na Mbunge wa Mwanga Mhe. Jumanne Maghembe akisalimiana na wakazi na viongozi wa Chama Mkoani Rukwa Ndugu Emanuel Seleman m-NEC (katikati) pamoja na Mzee Abdillah(wa kwanza kulia) waliokuja kuwapokea uwanja wa Ndege wa Sumbawanga mjini, Mhe. Maghembe ameongozana na Mhe Nape Katika Ziara yake hiyo.
Nape akisalimiana na wenyeji wa Sumbawanga waliojitokeza uwanja wa Ndege kumpokea. Katika Ziara yake hiyo Mheshimiwa Nape ameongozana na Viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mhe. Mwigulu Nchemba(katibu wa NEC- Uchumi na Fedha) Mhe. A. Mwanry (NW Tawala za Mikoa), Prof Jumanne Maghembe, Mb (Waziri wa Maji), Mhe. Benedictor Ole Nangoro Naibu Waziri wa Ujenzi., Dr Tizeba Charles (Mb,Nw Uchukuzi) Adam A. Malima(Naibu Waziri Kilimo)
Bi Rahel Ndegeleke Katibu wa Mkoa wa Rukwa, Mwigulu Nchemba(Mb) katibu wa NEC Uchumi na Fedha (katikati) na Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na Uenezi (kulia) mara baada ya kufika katika uwanja wa Ndege wa manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
0 comments:
Post a Comment