Meneja wa bia ya Serengeti lager Bw. Allan Chonjo (katikati) akizumgumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa wanne wa Bajaj, pikipiki, Jenereta katika droo ya tisa ya promsheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL, inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini. kulia ni Meneja Mawasilino wa SBL,Mwakilishi kutoka bodi ya bahati nasibu ya taifa Bw.Bakari Maggid na shoto kabisa ni Muwakilishi wa kampuni ya PWC,Bwa.Tumainieli Marisa wakishuhudia tukio hilo.
**********
WASHINDI WENGINE WANNE WASHINDA ZAWADI ZA SBL,WAWILI WASHINDA GENERETA, MMOJA AJISHINDIA PIKIPIKI,HUKU MWINGINE AKIJINYAKULIA BAJAJ, ZAWADI ZOTE MPYA KABISA,
Ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL.
July3,2012, Dar Es Salaam:Kampuni ya bia ya Serengeti leo imeendelea na droo ya tisa katika promosheni inayoendelea ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hiyo nchi nzima ambapo kwa mara nyingine washindi wane wameweza kuibuka na ushindi katika droo iliyochezeshwa leo asubuhi.
Akiongea na wandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo hiyo, meneja wa bia ya serengeti lager bw. Allan Chonjo amesema “ni wiki ya tisa sasa ambapo tunaendelea na promosheni yetu ambayo bila shaka watanzania wengi mmekuwa mkishuhudia watanzania wenzenu wakijishindia zawadi mbalimbali nakukabidhiwa pale walipojipatia zawadi hizo’ naendelewa kuwasisitiza wateja wetu na watatnzania wote kwa ujumla kuwa bado zawadi zipo nyingi na kwambakila mmoja wenu anaweza kushinda kama vile ambavyo wengine wanajishinadia.
Washindi wetu katika droo hii ya tisa ni bwana Boaz Mtukula kutoka Mwanza ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Twiga Bancorp mywaji wa bia ya Tusker Lager na bwana Richard Valerian kutoka Dar Es Salaam anayefanya kazi Bandarini mywaji wa Tusker pia ambao wote kwa pamoja wamejishindia jenereta mpya kabisa, na bibi Rahma Ally mkazi wa Temeke jijini Dar Es Salaam ambaye amejinyakulia pikipiki mpya mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager na Bwana Richard Mbizi mkazi wa Kimara jijini Dar Es Salaam amejishindia bajaj mpya kabisa, zawadi zote kutoka SBL.
0 comments:
Post a Comment