Nafasi Ya Matangazo

July 27, 2012

Na Mwandishi Maalum, Abuja.
WAKE wa Marais waAfrika wametakiwa kuwajengea uwezo wanawake na watoto wa kike kwa kuhakikishakuwa wanapata elimu ya kutosha ambayo itawawezesha kushika nafasi za juu katikauongozi na hivyo kupunguza ukatilia wa kijinsia dhidi yao.

Wito huo umetolewa jana na Raiswa Malawi Joyce Banda wakati akifungua  mkutanowa saba wa wake wa marais wa Afrika uliozungumzia masuala ya amani baraniAfrika uliofanyika mjini Abuja nchini Nigeria.

Rais Banda alisema kuwa ukatiliwa kijinsia kwa wanawake na watoto ni matokeo ya kukosekana kwa elimu na amanikatika nchi,  jambo la muhimu nikuwajengea uwezo wa kielimu na kiuchumi ili waweze kutambua haki zao za msingi.

“Kila mmoja wenu katika nchiyake anafanya kazi ya kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata elimu lakinihiyo pekee haitoshi bali mnatakiwa kuweka nguvu zaidi katika kuimarisha amani ndaniya nchi zenu kwani bila nchi kuwa na amani ukatili wa kijinsia utazidikuendelea”, alisema Banda.

Rais Banda aliendelea kusemakuwa wanawake wapewe nafasi katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro wasiachwewanaume peke yaokufanya kazi hiyo kwani nchi ikikosa amani waathirika wakuu ni wanawake nawatoto ambao wengi wao wanauawa na wengine wanafanyiwa ukatili wa kijinsiaikiwemo kubakwa.

Kwa upande wake  Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alisema kuwanchi za Afrika lazima zifanye jitihada kubwa za kuondoa vikwazo ambavyovinawazuia wanawake na watoto wa kike kushindwa kutimiza ndoto zao. Wanawakewanatakiwa kutobaguliwa bali kupewa fursa sawa ya kushiriki katika elimu, siasana uchumi.

Aliendeleakusema kuwa usawa wa kijinsia unatakiwa kuwepo barani Afrika kwa kuunga mkono nakutengeneza mazingira ya kuwainua wanawake kiuchumi na kuhakikisha kuwa wanawakehao wanaishi mazingira salama.

Mkutanohuo wa siku mbili unahudhuriwa na wake wa marais kutoka nchi mbalimbali BaraniAfrika akiwemo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Posted by MROKI On Friday, July 27, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo