Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2012

Kikosi cha mashabiki wa timu ya Man City wakiwa katika picha ya pamoja wakishangilia ushindi wao  mnono wa kuibuka kinara wa tamasha la Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2012,lililofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Nyamagana jioni ya leo jijini Mwanza.Mashabiki wa timu hiyo baada ya kunyakuwa ushindi huo wa jumla kati ya timu 9 za mashabiki zilizoshiriki shamra shamra hizo,pia walipewa zawadi ya kreti mbili za bia aina ya Serengeti sambamba na fedha taslim sh laki tano.Katika ulinganisho wa mwaka jana timu ya Real Madrid ilibeba kombe la tamasha hilo.
 Meneja mauzo Mkoa wa Mwanza,Octavian Migire pichani shoto akiwakabidhi mashabiki wa timu ya Real Madrid kreti moja ya bia aina Serengeti na kiasi cha fedha taslim sh laki tatu,mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindano ya  tamasha la Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2012 kwa jiji la Mwanza.
Mashabiki wa timu ya Man City wakipeana mkono wa pongezi na baadhi ya waratibu na wadhamini wa tamasha hilo,Kutoka kusoto ni Bahati Sigh kutoka Serengeti,Octavian Migire (sbl) sambamba na mratibu wa tamasha hilo ,Shaffih Dauda kutoka Clouds FM.
 Wakifutilia mtanange.
 Washabki mbalimbali wakifuatilia michuano hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Benchi la ufundi.
 Shabiki wa timu ya Chelsea akimtoka shabiki mchezaji wa timu ya Barcelona
 Hata kama shabiki,lakini kufungwa nako noma..!
 Golikipa wa timu ya Real Madrid akijaribu kuchupa kuokoa shuti kali la mpira lililoelekezwa golini kwake.
 Waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta Soka bonanza,Gsengo  na Shaffih Dauda wakijadiliana jambo.
Wadau mbalimbali wa vilabu vya nje hapa nchini wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri ndani ya uwanja wa Nyamagana,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta soka bonanza 2012.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza,wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta soka bonanza 2012 ndani ya uwanja wa Nyamagana.
Mratibu Mkuu wa tamasha la Serengrti Fiesta soka Bonanza,Shaffih Daudi akitoa muongozo wa mashabiki wa timu ya Barcelona na Chelsea,kabla ya kuanza kupambana vikali ndani ya uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza jioni ya leo.
Anaitwa Albert G Sengo a.k.a Gsengo ambaye alikuwa ni sehemu ya uratibu wa mchakato mzima wa tamasha la Serengeti Fiesta Soka bonanza 2012,pichani akizungumza machache wakati mashabiki hao wa vilabu mbalimbali walipokuwa wakichuana
Posted by MROKI On Monday, July 09, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo